MBOWE : NIMESHTUSHWA NA TAARIFA ZA KUTWALIWA KWA JABALI LA MAGEUZI TANZANIA, MAALIM SEIF |Shamteeblog.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa ameshtushwa na taarifa za kifo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kilichotokea hii leo na kutoa pole kwa familia yake.


Mbowe ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, masaa kadhaa tu tangu kifo cha Maalim Seif, kitangazwe na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi.

"Nikiwa hapa Dubai, UAE, nimeshtushwa na taarifa za kutwaliwa kwa Mhe. Sharif Hamad, jabali la mageuzi Tanzania, Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, natoa pole nyingi kwa familia, chama chake, Wazanzibari na Watanzania wote, kwake tumetoka na kwake tutarejea. Amin", ameandika Mbowe.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post