SERIKALI IMESEMA ITAHAKIKISHA MALENGO YA MKULIMA YANAFANIKIWA |Shamteeblog.

Na Mwandishi Wetu - Dodom


SERIKAI imesema kuwa ipo tayari WAKULIMA kuunga mkono na kutoa kila aina ya msaada unaohitajika ili kuhakikisha kwamba malengo ya wakulima yanafanikiwa hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthon Mavunde wakati akifunga maonesho ya wiki ya mavuno yaliyoandaliwa na kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini ( JATU PLC)

"Dodoma ni makao Makuu mahitaji yanaongezeka kwahiyo hata wakulima waongezeke na wajikite katika kilimo biashara ili kuondokana na ule utamaduni wa kulima mtama na mahindi siku zote fursa za kiuchumi zipo kwenye masuala ya kilimo cha biashara nitafurahi nikiona makundi ya kina mama,vijana na watu wenye ulemavu wakishiriki" Amesema Mavunde

Amesema muamko wa vijana umekuwa mkubwa katika kilimo tofauti na zamani ambapo kupitia mikopo ya halmshauri vijana wamewezeshwa fedha na wanaenda kufanya kilimo hivyo kampuni ya JATU itumie fursa hiyo kutoa elimu kwa vijana namna ya kulima kilimo cha kisasa. "

"Tunashukuru sana kwa maonesho haya ya JATU kufanyika jijini Dodoma tunaamini kwamba maonesho haya yataenda kubadilisha fikra na mtazamo ya wakulima wetu na hasa katika kuwekeza katika kilimo biashara na namna gani wanaweza wakafanya kilimo cha kisasa na hasa kwa sasa ambapo kilimo mboga mboga kimeonekana kushika kasi" Amesema Mavunde

Kwa upande wake Meneja kutokaTaasisi ya JATU Mohamed Simbano amesema kampuni hiyo ilianzishwa na vijana wa kitanzania ambao ni wahitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam lengo likiwa ni kuhakikisha ustawi wa maisha ya watu kiafya kutokana na bidhaa bora na asilia zinazotokana na kampuni hiyo.

“Pia inatoa suluhisho katika kupunguza umasikini kwa kutumia ipasavyo rasilimali watu kilimo cha kisasa na shughuli za viwanda pamoja na kugawana faida na mlaji wa mwisho”amesema Simbano.

Akizungumzia kuhusu kufunga maonesho hayo Simbano amesema wao kama JATU wanafanya kilimo kiwe sehemu ya kitega uchumi na si kuwa shughuli ya wazee mara baada ya kuustafu na kwa kipindi cha maonesho ya wiki moja wameweza kutembelewa na wakulima na wajasiriamali elfu 9 wakitaka kujifunza namna ya kulima kisasa.

"Kuhitimisha kwa maonesho hayo sisi kama JATU tunaenda kufanya tathimini tunaenda kuhakikisha kwamba tunaenda kujiridhidha wenyewe Sisi tutaendelea kutengeneza na tunaendelea kuwasisitiza vijana tuwe wamoja katika kuleta maendeleo ya nchi yetu" amesema Simbano.

Amesema kama kampuni wameambatana na maafisa ugani kwahiyo watu waliokuwa wakifika katika maonesho hayo walikuwa wanatatua changamoto zao kuhusu aina ya kilimo wanacholima.

"Lengo letu ni maeneo yote kujifunza namna ya kuimarisha na kuchochea ukuwaji wa sekta ya kilimo kama ilivyo sera ya kilimo na mikakati ya serikali katika kuhimiza taasisi kuweka nguvu katika kilimo kwa kuwa ndo sekta inayochangia katika sehemu kubwa ya pato la taifa”

"Tunaishukuru sana Serikali na uongozi wa jiji la Dodoma kwani mapokeo yamekuwa mazuri tofauti na mikoa mingine tulipowahi kwenda hapa mapokezi na muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa sana wa kuja kujifunza " amesema Simbano

Hata hivyo maonesho hayo ya kilimo kanda ya kati yanamefungwa tarehe 20 october huku yakiwa yamebebwa na kauli mbiu isemayo" wiki ya mavuno anza na ekari moja".




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post