Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwapatia fedha Tsh. 420,000,000/= za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa dhidi ya mapambano Uviko 19 kwa ajili ya kujenga Madarasa 21 kwa shule ya msingi na za Sekondari kwa kata zote za Tarafa ya Mihambwe.
"Kwa niaba ya Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tunamshukuru sana sana Rais Samia kutupatia fedha kujenga Madarasa 19 ya Sekondari na Madarasa 2 shikizi kwa shule ya msingi ya Mwenge. Ukamilifu Madarasa haya 21 yataondoa kabisa tatizo la uhaba wa Madarasa halitakuwepo mpaka mwaka 2025. Tunamuhaidi Rais Samia kumaliza ujenzi huu kwa wakati tena kwa ubora unaolingana na thamani ya fedha." Alisema Gavana Shilatu
Hayo yamebainishwa na Gavana Shilatu kwenye mkutano na Wananchi uliofanyika Kijiji cha Mwenge B uliohusisha vijiji vya Mwenge A na Mwenge B vilivyopo kata ya Kitama kwa ajili ya kutambulisha mradi kwa jamii na kuchagua Wajumbe Wananchi watakaoingia kwenye Kamati za mradi wa ujenzi.
"Kwenye Tarafa ya Mihambwe tutahakikisha mradi unakuwa shirikishi na kwa uwazi zaidi ndio maana tunawajumuisha Wananchi kwenye Kamati zote tatu za miradi ya ujenzi. Tunawataka Wananchi mjitolee nguvu kazi zenu ili tukamilishe Madarasa haya pamoja na kuweka Madawati yake kabisa ili Watoto wetu wasome kwenye mazingira mazuri." Alisisitiza Gavana Shilatu
Kwenye Mkutano huo Gavana Shilatu alijumuika pamoja na Afisa elimu msingi wa wilaya, Diwani kata ya Kitama, Uongozi wa kata, vijiji, bodi na Uongozi wa shule.
By Mpekuzi
Post a Comment