*Katibu Mkuu CCM awahakikishia wananchi deni hilo lazima lifutwe,hawawezi kukaa kimya
Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Mwanga
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Daniel Chongolo amesema amesikitishwa na taarifa za kuelezwa kwamba Kuna zahanati zilizopo Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro hazina hazina dawa eti kwasababu zinadaiwa na Bohari ya Dawa( MSD).
Amesema atahakikisha changamoto hiyo inafanyiwa kazi haraka na MSD ili wananchi wapate huduma za matibabu ya afya ikiwemo ya kupata dawa katika zahanati hizo huku akieleza kama kuna deni ikishaeleweka sababu yake lifutwe na waanze upya.
Akizungumza na wananchi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara za kukagua utekelezaji wa Ilani pamoja na kuangalia uhai wa Chama ,Chongolo amesema katika kushughulikia changamoto ya kukosekana dawa kwenye zahanati atakwenda kukaa na watalaamu wamueleze kuhusu Zahanati zote zilizopo Ugweni zinadaiwa shilingi ngapi.
"Tumeahidi kuhudumia na kulinda afya za wananchi wetu na dawa ni sehenu muhimu katika kulinda afya zetu,hatuwezi kuwa tunapiga hadithi kwenye maisha ya watu ,hata mwananchi mmoja akipotea ni hasara kubwa hatuwezi ruhusu mwananchi apoteze maisha eti kwasababu imekosekana dawa ya kumtibu na ugonjwa unatibika
"Ni lazima sisi tuwe daraja la kuhangaika na hilo na Kwa kweli nimesikitika kusikia kwamba dawa haziji wasababu kuna deni , hiyo haikubaliki na hiyo sio sawa ,kama kuna changamoto tutafute na kuitatua lakini tusikatishe huduma kwa wananchi,"amesema Chongolo.
Ameongeza kwamba amepata taarifa kuna wananchi ana bima kubwa na anapoenda hospital na bima yake bima inalipiwa fedha lakini anaambiwa hakuna dawa katika zahanati kwasababu kuna deni ."Kwanini usipeleke dawa wakati inalipiwa kwasababu hiyo bima ipo na inalipiwa kupitia NHIF.
"Na hiyo fedha inarudi kukulipa MSD ,kwanini iendelee kuwa tatizo kwa kiwango hicho ,hilo halikubaliki lazima twende tukakae na wao na mimi nipongeze MSD kwa jitihada zinazoendelea kufanyika,kulikuwa na changamoto ambazo zimeanza kufanyiwa mabadiliko.
"Tayari pale MSD amepatikana Mkurugenzi mpya tayari na Wizara inaendelea kupanga mifumo, na sisi hatutaki kujipanga kwao tunataka matokeo kwa wananchi.Tunataka dawa huku na hiyo ndio kazi niliyotumwa na Mwenyekiti kuja kuifanya huku ya kuja kujiridhisha na huduma kwa wananchi,"amesema Chongolo.
Amesisitiza na pale kwenye changamoto lazima waziseme kwani hawawezi kuwa Chama kinachosimamia Serikali halafu wanapiga makofi mahali ambako hakuleti tija."Tutakuwa wa ajabu kwasababu kesho tutajua kuulizwa tulipewa dhamana mbona dawa hakuna ,mbona kituo cha afya hakuna.
"Mbona hakuna barabara ,mbona hamkumfanya hiki,hakumfanya hiki ,hatuko tayari kuulizwa maswali hayo.Niwahakikishie tunakwenda kubanana huko kujua changamoto ya yale madeni ambayo yanadaiwa kwenye zahanati zenu,tujue yako kwa kiwango gani, tujue sababu gani na baada ya kujua sababu tutafute suluhisho kuhakikisha madeni yanafutwa ili tuanze upya kuwa na uhakika wa dawa kwenye zahanati zetu ,"amesema Chongolo.
Diwani wa Kata ya Vuchama Baraka Maradona akieleza changamoto ya dawa katika zahanati ya kijiji hicho,Ugweno Mwanga mkoani Kilimanjaro mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo
Baadhi ya Wanachama wa CCM pamoja na Wananchi wa kijiji cha Vuchama-Ugweno wilayani Mwanga wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alipokuwa akizungumza nao leo Agosti 6,2022.
By Mpekuzi
Post a Comment