Mtunzi : Aidan Shamte
No. 0679784428/0742621952
Ninachokumbuka awali nilimueleza kabisa kuwa kazi yangu hainipi wakati wa kuwa na mpenzi na kumtendea haki. Hapa ni baada ya kuniuliza eti kwa nini sina mpenzi wakati nilikuwa nimejipanga kimaisha tayari!!
Mazoea yakapiga hatua mbele akanisisitiza kuwa yeye yupo tayari kuwa na mimi katika hali hiyohiyo akadai anaielewa kazi yangu hivyo atakuwa mvumilivu lakini hasahasa atakuwa muaminifu kwangu!!!
Nikashawishika nikamkaribisha nyumbani kwangu!!
Ile siku niliyomkaribisha akainasa mimba!!
Na hapo nikatangaza ndoa lakini kiukweli moyoni mwangu nilikuwa sijapanga iwe hivyo!! Ilibidi tu kwa sababu alikuwa mjamzito!!!Mazoea yakapiga hatua mbele akanisisitiza kuwa yeye yupo tayari kuwa na mimi katika hali hiyohiyo akadai anaielewa kazi yangu hivyo atakuwa mvumilivu lakini hasahasa atakuwa muaminifu kwangu!!!
Nikashawishika nikamkaribisha nyumbani kwangu!!
Ile siku niliyomkaribisha akainasa mimba!!
Maisha yangu na bi Hindu Kimbe yakanifanya nisahau kuwa hapo awali sikuwa nahitaji kuingia katika ndoa.
Nilijitahidi sana kadri ya muda na uwezo wangu kumwonyesha kuwa ninampenda sana. Hakika alikuwa ni yeye tu katika moyo wangu na sikuwaza hata siku moja kumsaliti.
Ubaharia ukaniweka majini masaa mengi kuliko katika ndoa yangu!!
Baada ya miezi kadhaa akiwa mjamzito mke wangu akaanza kulalamika kuwa anakuwa mpweke sana kuwa mwenyewe nyumbani.
Akaomba nimpe ruhusa mdogo wake wa kike aje kuishi naye pale na kuwa anamsaidia kazi za hapa na pale.
Nikamruhusu bila kusita, sikuona tatizo kabisa yeye kuja kuishi pale akiwa na mdogo wake.
Maisha yakaendelea!!
Baada ya kujifungua mdogo wake yule akaendelea kuwepo pale akimsaidia dada yake kulea mtoto na mimi nikiwa nimetingwa na shughuli zangu za ubaharia.
Tabia za mke wangu zikaanza kubadilika miezi mitatu baada ya kuwa amejifungua.
Alikuwa si mchangamfu sana na kila mara alikuwa akiniomba ruhusa za kwenda mahli kadha wa kadha.
Baharia mimi nilizaliwa nikiwa si msemaji sana na hakika sikupenda kujibishana hili hata bosi wangu kazini alikuwa akilifahamu fika.
Hivyo nilikuwa nikimruhusu kila aliponiomba kwenda mahali.
Baada ya muda zile ruhusa hazikuombwa tena, nikajidanganya kuwa huenda mke wangu ametambua kuwa sijapendezwa na tabia zake hivyo ameamua kubadilika.
Lakini haikuwa kama nilivyodhani!!
Afya ya mtoto wangu ikaanza kulegalega wakati matumizi nilikuwa natoa ya kutosha.
Nilishangaa anazidio kupungua uzito kila kukicha nilipomuuliza mke wangu akadai kuwa ni hali ya kawaida tu ile inayotokea kwa watoto.
Ningebisha kitu gani wakati sijawahi kuwa mzazi hapo kabla!!
Maisha yakaendelea lakini jicho langu likawa linapata mashaka juu ya afya ya mwanangu na ule ukimya wa mke wangu!!
Sikuwahi kuwa na mazoea ya karibu sana na mdogo wa mke wangu yaani shemeji yangu hivyo zaidi ya salamu hapakuwa na jingine kati yetu.
Lakini macho yake siku za awali na ya sasa yalikuwa tofauti kabisa. Ni kama kuna kitu kilikuwa kinaendelea na hakuweza kunieleza.

Ilifikia kipindi nikapata dharula kazini na kuamriwa kusafiri na meli ya mizigo kuelekea uingereza. Nilimueleza mke wangu kuwa sijapendezwa na safari ile lakini itanilazimu tu kwenda huko.
Mke wangu alikuwa amenitambua tayari kuwa sipendelei sana kujibizana hivyo nisingeweza kuipinga safari ile.
Nikamuaga yeye na mtoto na kumwachia mke wangu kiasi cha pesa za kutosha kwa matumizi ya hapa na pale katika kipindi hiki ambacho sitakuwepo.
Nikaondoka huku nikimkumbusha kuwa ninampenda sana naye akanijibu kuwa ananipenda pia!!

****
Nilipofika bandarini nilimkuta bosi wangu akiwa ananisubiri.
Akaniuliza, “Khalid ni kweli upo tayari kusafiri na chombo…..”
Najua aliniuliza kwa sababu mimi sikuwa muongeaji sana na sikujua kukataa!!
Nikamueleza kuwa akipatikana mtu wa kwenda badala yangu itakuwa jambo jema sana.
Bosi wangu akatabasamu kisha akafungua mkoba wake na kutoa bahasha akanikabidhi kisha akanikumbatia.
“Umepata likizo ya miezi mitatu Khalid, u mfanyakazi mwenye nidhamu ya kazi sana nenda ukalee mtoto wako Khalid!!” alinieleza yale huku akinigongagonga bega langu!!
Nilifurahi sana hakika.. nikamshukuru kisha nikaondoka kurejea nyumbani!!
Yalikuwa majira ya saa kumi jioni!!
Sikumkuta mke wangu nyumbani, nikamkuta mtoto wetu mchanga yule akiwa analia mikononi mwa mama yake mdogo yaani shemeji yangu!!
“Mama yake ameenda wapi tena?”nilimuuliza baada ya kuwa tumesalimiana.
“aliniaga kuwa anaenda saluni…” alinijibu huku akiendelea kufanya jitihada za kumbembeleza mtoto.
Sikuzungumza zaidi nikaingia chumbani na kujilaza. Nikiwa napanga maneno ya kuzungumza na mke wangu ili atambue umuhimu wa kuwa karibu na mtoto hasahasa mtoto mchanga!!
Hakurejea hadi majira ya saa moja na nusu usiku!!
Saluni gani hiyo? Nilijiuliza!!
Alipoingia chumbani macho yangu yakakitazama kichwa chake, hakikuwa na mabadiliko yoyote yale.
Bila shaka hakuwa saluni. Kwa maksudi sikumuuliza.
Tulisalimiana nikamueleza kuwa nimepata likizo ya malipo kazini na nitakuwa nyumbani miezi ipatayo mitatu.
Mke wangu aliipokea taarifa ile kwa tabasamu hafifu tofauti na nilivyotarajia. Sikujali kabisa kuhusu hilo nikaingia bafuni kuoga kisha nikaingia kitandani nikapitiwa na usingizi.
Nilikuja kushtuka majira ya saa nane usiku mke wangu akiwa hoi amelala. Niliiona simu yake ambayo nilikuwa na uhuru nayo na kamwe sikuwahi kuwa na mipaka katika hili.
Nilipoitazama nikakuta imefungwa kwa namba za siri.
Si kwamba haikuwahi kuwa na namba za siri la! Ilikuwa na namba za siri lakini nilipoziingiza haikufunguka!!
Alikuwa amebadilisha namba za siri!
Kwanini? Nikajiuliza na kisha nikairejesha simu mahali ilipokuwa nikatabasamu na kujifunika shuka!!

Asubuhi siku ilianza katika namna ya pekee, mke wangu hakuwa na amani na kila muda alikuwa akitembea na simu yake!!
Na mara kadhaa alizopigiwa simu alikuwa akienda kuzungumza mbali nisiweze kumsikia.
Nilibaki kutabasamu huku nikiamini kuwa mke wangu alikuwa anajaribu kuweka siri katika jambo ambalo limekuwa zito tayari.
Nilimuacha aendelee kutapatapa na sikumuuliza lolote lile nilijifanya sijaiona ile tofauti.
Siku hiyo ikapita!!
Ikaingia siku ya pili, asubuhi sana mke wangu akaniomba ruhusa kuwa anahitaji kwenda kwa rafiki yake.
Sikumuuliza kufanya nini nikamruhusu. Natambua kuwa alishtuka sana lakini nikajifanya simuoni.
Akajiandaa akaondoka!!!
Alirejea baada ya masaa manne akanikuta nikiwa pamoja na mdogo wake tukizungumza huku tukisaidiana kumbembeleza mtoto. Akafika na kutupa pole kisha akamchukua mtoto na kumnyonyesha mtoto akanyamaza na kulala.
Siku iliyofuata alitembelewa na mgeni nisiyemjua, alinitambulisha kuwa yule ni rafiki yake tu. Na kisha wakaenda kuzungumza kando nikaona kuna kitu walipeana.
Kama kawaida sikutilia maanani!!
Usiku wa manane alivyokuwa amelala, nikapekua mle ndani na kufanikiwa kuukuta mzigo aliopewa na yule rafiki yake.
Ilikuwa ni bahasha na nilipoifungua ndani zilikuwa ni pesa nyingi sana. Na juu pakiwa na kikaratasi kilichoandikwa neno la kiingereza lililomaanisha ASANTE!!
Nikatabasamu na kujiuliza kwani lini mke wangu ameanza biashara, na ni biashara gani hiyo ambayo sikuhusishwa hata kidogo katika kutoa mtaji.
Kama sikuhusishwa basi iwe isiwe itakuwa ni biashara haramu tu!!
Na hapo nikakoma kutabasamu nikafanya maamuzi!!
Siku iliyofuata nilitegea hadi aliponiomba ruhusa kuwa anaenda katika kikao cha wanawake. Nikamruhusu lakini nikiwa na wazo langu moja kuu kichwani.
Saa zima baada ya kuondoka nilikuwa nimefanikiwa kumbembeleza mtoto wangu hadi akasinzia nikamlaza katika kitanda chake kisha nikamfunika kabisa ili asisumbuliwe na nzi!!
Baada ya hapo nilienda chumbani kwangu kisha nikapaza sauti na kumuita Felister ambaye alikuwa ni shemeji yangu!!
Alifika hadi mlangoni na kuniuliza nilikuwa na haja gani. Nikamsihi aingie ndani nimuagize, kwa sababu alikuwa ananiheshimu na hatukuwa na mazoea hatarishi aliingia.
Alipoingia tu nikaufunga mlango.
Na hapo nikatoa panga kali sana uvunguni!!
“Felister nimewahi kukugombeza hata mara moja tangu unifahamu!!”nilimuuliza.
“Hapana shem..” alijibu huku akiwa anatetemeka sana.
“Umewahi kusikia nampiga dada yako hata siku moja”
“Hapana kaka aah shemeji sijawahi kusikia..”
“Vizuri, mimi si mtu wa kupenda masumbufu yanayoepukika, basi na wewe ntapenda uwe kama mimi. Usipende kuficha masumbufu ambayo yanaepukika, lakini kama ukisema uyafiche leo utanishangaa sana…. Utanishangaa kwa sababu utakuwa mtu wa kwanza kushukiwa na hasira yangu!!! Nahitaji kujua mke wangu yaani dada yako mambo gani anayafanya nyuma ya pazia yaani anayafanya na mimi sijui na wewe unayajua kuwa si mambo mazuri!!!” nilimuuliza kisha nikalificha lile panga ili aistishike zaidi.
“Shemeji…”aliniita….. nikaitika.
“Hukuwa na haja ya kutumia panga wala kitisho cha aina yoyote niliingojea siku hii ifike, siku ya kuzungumza na wewe…”
“Felister wajua ni kiasi gani nampenda dada yako hadi nafanya mambo ya kipuuzi kama haya tambua kuwa nimechanganyikiwa kabisa, kuna mambo ananifanyia dada yako Felister yapo mambo machafu, tazama tuna mtoto mchanga lakini… lakini ananifanyia upuuzi. Felly niambie iwapo kuna mwanaume anampenda na kumjali dada yako kuliko ninavyofanya mimi nami nitawaacha huru niambie tu shemeji yangu!!” sasa nilikuwa mtaratibu na nilizungumza kwa masikitiko makubwa!!
Felister aliketi chini kisha akanieleza mambo lukuki, yaani Hindu anafikia hatua ya kuwaleta marafiki zake wa kiume pale nyumbani, bora japokuwa si afadhali., angekuwa mmoja basi yaani wanaume si chini ya watatu tofauti tofauti na kisha kumpa onyo mdogo wake asije akathubutu kuzungumza lolote lile akadai eti anafanya vile ili apate pesa za kumpa mama yake nyumbani kwa sababu mimi simpatii pesa kabisa na siijali family yao.
Safari zote za kila siku ni kwa wanaume na hata ile pesa niliyoifuma ilikuwa ni ujira baada ya kwenda kwa mwanaume.
Maneno ya Hindu yaliniumiza sana nikatamani mke wangu atokee na niweze kumwadhibu vikali.
Hindu alikuwa hajamaliza, akanipigilia msumari wa mwisho.
“Shemeji hata huyu mtoto si wako ulimuona da Hindu akiwa ni mjamzito!!”
Ndugu msikilizaji niliishiwa nguvu nikaketi chini, damu zikaanza kunitoka puani nikawa naunguruma mithiri ya Simba. Hasira ilikuwa imenipanda sana.
Nikiwa bado nimeketi pale damu ikinitoka mara mlango ukagongwa!!!
Ni heri asingekuja wakati ule yule mwanamke, ni heri angepotea kabisa huenda na akili yangu ingekaa sawa na hasira kupoa.
Mlango ulikuwa unagongwa na Felister alipoufungua alikuwa ni Hindu.
Lile panga halikuwa mbali.
Nikafyatuka na kulichukua Felister hakuweza kunizuia.
Nilimcharanga vibaya sana Hindu!!
Nilimcharanga uso na mikono yake!!!
Kisha sikujua lililotokea hadi nilipojikuta hospitali nikiwa na pingu mkononi.
Baada ya majumaa kadhaa nilikuwa katika safari ya kuelekea gerezani.
Nikatumikia kifungo cha miaka saba jela.
Nipo tena uraiani baharia wa zamani mimi, zungumza nami kila aina ya maongezi lakini ukitaka kunifukuza kijiweni yasifie mapenzi.
Niombe kila aina ya ushauri ila la usiniombe ushauri wa mapenzi nitakujaza sumu bure!!
Zile alama za mapanga hazikuwahi kuisha katika mwili wa yule mwanaharamu ni jambo hilo tu linalonipa faraja kwa sasa!!!

MWISHO
Post a Comment