Mgahawa Waporomoka na Kusababisha vifo China |Shamteeblog. |Shamteeblog.

Mgahawa Waporomoka na Kusababisha vifo China |Shamteeblog.

Mgahawa wa ghorofa mbili umeporomoka na kusababisha vifo vya watu 13 Shanxi nchini China.

Kulingana na kituo cha televisheni cha taifa nchini humo CCTV, tukio hilo limetokea katika mji wa Shiangfen, kilometa 630 kusini magharibi mwa mji mkuu Beijing.

Watu 30 wameokolewa baada ya kuwa wamefunikwa na kifusi huku wanne kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Mamia ya maafisa wanaendelea na shughuli za utafutaji na uokoaji, Hakuna taarifa kamili kuhusu sababu kuu ya kuanguka kwa jengo hilo.

from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3lw4lKl

via Mpekuzi https://ift.tt/2ENg2vn
August 30, 2020 at 09:26AM

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post