WANANCHI wa kata ya Tambani wameombwa kukipa kura nyingi chama cha mapinduzi CCM ili waweze kurekebishiwa miundo mbinu yao ya barabara ambayo nichangamoto pamoja na daraja la kifaulongo lilopo katika kata hiyo ambalo limevunjika kutokana na mvua nyingi zilizonyesha kipindi kilichopita.
Akizungumza wakati wa kampeni akiwa katika kijiji cha Tambani, kata ya Tambani wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani,Mgombea ubunge jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega amewahakikishia wananchi hao kwamba kipindi cha masika kijacho daraja hilo ambalo ni kiunganishi kati ya wilaya ya Temeke na mkuranga litakuwa limerekebishwa.
Ulega ambaye pia ni naibu waziri wa mifugo Na uvuvi ameongeza kuwa Kazi iliyofanywa na serikali miaka mitano nikubwa kwani ilishajenga daraja hilo llakini kwa bahati mbaya lilikatika kwahiyo amewahakikishia wananchi hao kwamba kazi iliyobaki kwa marekebisho ni ndogo na eneo hilo litapitika kipindi chote kiangazi na masika.
Aidha mgombea huyo amesema anajua kama barabara za Tambani ni changamoto zinamandimbwi na mabonde lakini ameahidi kuwa kipindi kijacho zote zitarekebishwa ziweze kupitika vizuri
Akizungumzia suala la umeme kwa vijiji vitatu vya tambani ulega amesema kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ya 20/25 kila eneo umeme utafika na kwa kijiji cha Tambani A mpaka ifikapo sept 29 mkandarasi atakuwa amekabidhi kazi.
Hata hivyo Ulega amefanya kampeni Katika vijiji vitatu vya kata ya Tambani ambavyo ni kijiji cha tambani, Mlamleni na Lunzando na kuwataka kukichagua chama cha Mapinduzi kwa kura nyingi ili waendelee kuboreshewa huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu, umeme na maji
Akiwa kijiji cha Lunzando mgombea wa CCM ameahidi kutoa mifuko miatatu ya saruji kusidia ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho endapo akishinda ili wananchi hao wandokane na adha katika hupatikanaji wa huduma ya afya.
Kwa upande wake aliyekuwa diwani wa tambani kipindi kilichopita Ally Mtamilwa amekipongeza chama cha mapinduzi ccm chini ya Daktari John Pombe Magufuli kwa yale walioyoyafanya kata ya tambani ndani ya miaka mitano, ikiwemo umeme, elimu afya na ujenzi wa daraja la kifaulongo ambalo serikali ilitoa milion 500 na kuwataka wananchi kuwa na imani na ccm.
Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo ya Kijiji cha Tambani Kata ya Tambani katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwenye viwanja vya Mwanambaya. Wakati wa kunadi sera za chama chake.Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo ya Kijiji cha Tambani Kata ya Tambani katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwenye viwanja vya Mwanambaya. Wakati wa kunadi sera za chama chake.Wananchi wa kata ya Tambani wakimsikiliza Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega (hayupo pichani).Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi leo ya Kijiji cha Tambani Kata ya Tambani katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwenye viwanja vya Mwanambaya. Wakati wa kunadi sera za chama chake.
By Mpekuzi
Post a Comment