Habari njema kwa wateja wa Zantel, wawezeshwa kulipia bili za maji kwa Ezypesa |Shamteeblog.

Zanzibar, Septemba 25,2020

Kwa sasa wateja wa Zantel wanaweza kuipia bili za maji kiurahisi zaidi kwa njia ya Ezypesa baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), mfumo wa kidigitali zaiid wa kufanya malipo.

Hatua hiyo itaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato huku ikiwapunguazia wateja adha ya kusafiri umbali mrefu ili kulipia huduma hiyo muhimu.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Zawa, Mussa Ramadhan alipongeza hatua hiyo akieleza kuwa itasaida katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja visiwani Zanzibar.

“Mkakati wetu ni kuendeleza na kutoa huduma ya maji ya uhakika na nafuu kwa wateja wetu, hivyo ushirikiano wetu na Ezypesautasaidia katika kufikia malengo yetu kwani utaongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kuwapunguzia wateja mzigo wa kutembea umbali mrefu kwani kwa sadsa kila kitu kitafanyika kwa simu,” alisema.

Huduma hiyo ni suluhisho katika kuongeza kasi na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato hivyo kusaidia mamlaka kuwa na uwezo wa kuboresha miundimbinu ya maji na kuwafikia watu wengi zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Khamis Mussa alisema hatua hiyo ni muhimu katika kutekeleza mkakati wa Zantel wa kuboresha Maisha ya watu kupitia huduma za Ezypesa ambazo zinawapa wateja wake uhuru na urahisi wa kupata huduma mbalimbali.

.Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Khamis Mussa akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza ushirikiano kati ya Zantel na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ili kuwawezesha wateja kulipia ankara kwa urahisi zaidi kwa njia ya Ezypesa. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za kifedha wa Zantel, Sakyi Opoku.Huduma hiyo itawawezesha wateja kulipia bili za maji muda wowote kwa njia ya simu.

“Kupitia Ezypesa tumejidhatiti katika kuboresha Maisha ya watu kwenye Nyanja mbalimbali ili kuwezesha urahisi wa upatikanaji wa huduma na mahitaji ya kila siku.Ushirikiano wetu na ZAWA ni hatua muhimu katika kuhakikisha wateja wetu wanalipia ankara za maji mahali popote,” alisema Mussa.

Aliongeza “Tofauti na njia za awali, kwa sasa hakuna haja tena ya kutembea umbali mrefu ili kulipia bili au usubiri mpaka maji yakatike kwa kuchelewesha bili, kwa simu yako tu unaweza kujihakikishai unapata huduma ya maji.”

Ni dhahiri kuwa maji ni rasilimali muhimu katika kuchochea huduma za kibiashara Pamoja na zile za majumbani.Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) inafanya jitihada kubwa kusimamia huduma ambayo hadi sasa imewafikia wateja 1,161,915 visiwani Zanzibar.

Ili kulipa bili, mteja wa Zantel atapiga *150*02# kisha 5 Malipo na Kisha 7 Kisha chagua 3 Bili za Maji kisha ZAWA na endelea na malipo kwa kuingia namba ya akaunti ya maji iliyopo kwenye bili yako na kiasi kisha thibitisha. Mteja atapata ujumbe (SMS) kwa malipo yaliyofanyika.

Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Zanzibar, Salama Aboud Talib akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ushirikiano kati ya Zantel na Mamalaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ili kuwawezesha wateja kulipia ankara za maji kirahisi zaidi kwa njia ya Ezypesa.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Al-Khalil Mirza na Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA, Mussa R.Haji.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post