Kuzaa Kulivyoigharimu Afya ya Muigizaji Sarafina...... |Shamteeblog.


Leleti Khumalo maarufu kama ‘Sarafina’ mzaliwa wa Afrika Kusini ambaye alizaliwa March 30,1970 na alipata umaarufu baada ya kuigiza filamu ya Sarafina mwaka 1992 na filamu hiyo kutambulika kimataifa hadi kumpatia tuzo mbalimbali.

Filamu hiyo inayohusu msichana (Sarafina) aliyekuwa na msimamo wa kuitafuta haki bila uwoga na kusimama katika maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukifanywa nchini Afrika Kusini.


Leleti kwa sasa aanasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaofahamika kwa jina la Vitiligo ambao umeathiri sehemu kubwa ya ngozi yake ikiwemo usoni na mikononi.

Kutokana na mahojiano mbalimbali aliyowahi kufanya na vipindi tofauti vya habari Leleti alisema kuwa kwa mujibu wa madaktari walimuambia kuwa endapo atafanya maamuzi ya kuzaa basi ugonjwa huo utaathiri sehemu kubwa ya ngozi yake, lakini Leleti hakujali hilo na aliamua kupata watoto.Kwa sasa Leleti ana watoto wawili mapacha aliozaa na mfanyabiashara Skhutazo Winston Khanyile.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post