Maalim Seif kutoa mikopo kwa wafanyabiashara |Shamteeblog.

 MWANDISHI WETU – ZANZIBAR 

MGOMBEA wa Urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesemaendapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atatoa mikopo kwa wafanyabiashara ili waweze kukuza bishara zao.

Alisema hayo katika viwanja vya Mkele Jimbo la Shauri Moyo Wilaya ya Mjini Magharibi wakati akiendeleza kampeni za nafasi hiyo visiwani humo. 

Alisema wafanyabishara ni watu muhimu katika nchi kwa hiyo katika Serikali yake atawaangalia vyema na yeyote aliyekuwa anataka kuwekeza au kufanya buiashara basi watakuwa na nafasi mkopo na kurudisha wenyewe kwa taratibu. 

“Kuna wafanyabishara wengine wanakuwa na biashara zao lakini kutokana na mtaji mdogo zinakufa, lakini katika Serikali nitakayoiongoza nitahakikisha mitaji imenyanyuka,” alieleza Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo. 

 Kwa upande wa wananchi wake ambao wana mawazo mazuri ya kuwekeza lakini hawana mitaji, mgombea huyo alisema ataweka taratibu nzuri za mikopo ili waweze kupata chanzo cha kuwekeza na baadae waweze kutoa ajira kwa vijana. 

“Tukifungua kampuni pamoja na viwanda ni msaada mkubwa kwa Serikali kwani wananchi wetu watapata ajira humohumo,” alieleza. 

Alisema nchi nyingi ambazo zimetumia utaratibu huo zimekuwa na wananchi walioajiriwa kwa asilima kubwa sana. 

Alieleza kuwa anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya biashara ni lazima aweke mipango madhubuti ya kufikia hatua hiyo. 

Munamo nyakati za asubuhi aalim Seif alifanya ziara ya kutembelea masokona leo ilikuwa zamu ya soko la Mikunguni na kuzungumza na wafanyabisha sehemu hiyo. 

Alisema anasikitka Viongozi wa CCM wanasema uchumi umepanda hali ya kuwa wananchi wan shida mpaka biashara zao zimekufa. 



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post