Na Mwamba wa Kaskazini
Mpaka leo tafiti mbalimbali zinampa Rais Dkt John Pombe Magufuli ushindi wa zaidi ya asilimia 85 katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu dhidi ya wagombea wengine.
Bila shaka, hili linatokana na uchapakazi wake pamoja na uzalendo wake kwa taifa hili.
YAPO MENGI YA KUJIVUNIA CHINI YA RAIS MAGUFULI
Kwa miaka Mitano iliyopita Tumeshuhudia Rais John Pombe Magufuli akiendelea Kuwa Mfuasi Mzuri wa Falsafa za Mwalimu Julius Nyerere ambaye Kupitia Dira ya Uongozi wake, alisisitiza sana Kujenga Taifa la Kijamaa na Kujitegemea.
Niendelee Kwa Kusema Kuwa Rais Magufuli Mara baada ya kuingia tu Madarakani ili Kujenga Taifa la Kujitegemea Kiuchumi alifanya yafuatayo na kuendelea kuyasimamia Kikamilifu; Ameboresha Ukusanyaji Mapato ya serikali yatokanayo na Kodi Kutoka Bilioni 850 Mwaka 2015 hadi Kufikia Trilioni 1.3 ( Disemba 2019 ) Fedha za Kitanzania na Kwa Mapato yasiyo ya Kodi Rais Magufuli amefanikiwa kwa Kiasi Kikubwa Kuboresha Ukusanyaji wake na Kuongezeka Kutoka Chini ya Bilioni 688 mwaka 2014/2015 hadi Kufikia Trilioni 2.4 Fedha za Kitanzania Mwaka 2018/2019
Aidha Rais Magufuli pia amefanikiwa sana Katika kudhibiti Matumizi yake na Kwa Kiasi kikubwa ameelekeza fedha hizo kuwahudumia Watanzania Kwa kuwaletea Maendeleo Katika Sekta zote. Rais Magufuli amefanikiwa Kwa Kiasi Kikubwa Kuimarisha Utendaji Kazi Serikalini, Maadili na Nidhamu Kwa Watumishi wote wa Serikali ( UMMA ) na Katika hili hakusita Kuchukua hatua za kinidhamu hadharani Kwa Watumishi Walioshindwa Kufanya Kazi kwa Weledi, Nidhamu, Maarifa na Uadilifu.
Rais Magufuli toka ameingia madarakani mwaka 2015 alituahidi Kulinda Raslimali za Taifa letu ili kuhakikisha Urithi wa Raslimali tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu zinabaki Kuwanufaisha Watanzania wote na hapa ningependa kuwakumbusha Watanzania Kwa kurejea katika lile Sakata la makinikia na Madini yetu kama mfano mmoja wapo.
Mosi kabisa, Mageuzi Makubwa sana yamefanyika Ikiwa ni pamoja na Kuanzisha Wizara Mahsusi ya Madini, Kudhibiti Utoroshaji na Usafirishaji wa Madini ghafi nje ya Nchi, Rais Magufuli ameanzisha Masoko ya Madini Kila Mkoa ambapo Kupitia hili Mapato yatokanayo na Madini sasa yamekuwa na yanaonekana wazi. Serikali ya Rais Magufuli kupitia Bunge la JMT ilitunga na kupitisha Sheria ya Kulinda Rasilimali za Taifa ya Mwaka 2017 ( The Natural Wealth and Resources Permanent Sovereignty Act, 2017 ) Ikiwemo Madini.
Kupitia Sheria hii, tumeshuhudiwa Kwa mara ya Kwanza Watanzania wanamiliki Rasilimali zao kwa Nguvu za Kisheria Kama akina Saniniu Laizer😅 Mzee wa Tanzanite.
Ni kupitia Sheria hiyo pamoja na Jitihada za Rais Magufuli na Serikali yake, wale Waliokuwa wanatunyonya “Mabeberu" Walisalimu Amri na Kukubali Kutulipa Watanzania Malipo ya Fidia ya *Dola za Kimarekani Milioni Mia Tatu ( us-dollars 300 Millions ) ambazo Kampuni ya Barrick ilikubali Kutulipa Kufuatia Majadiliano na Makubaliano na Tayari Dola za Kimarekani Milioni Mia Moja ( us –dollars 100 Millions ) tumekwisha lipwa.
Mafanikio mengine Kupitia Makubaliano ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick* ni pamoja na Kuanzishwa kwa Kampuni ya Twiga Minerals Company ambayo Serikali yetu inamiliki 16% na Kampuni ya Barick 84% .
Watanzania tunayo mengi sana ya Kujivunia Kama Taifa linalohitaji Kusonga Mbele Kimaendeleo, Kiuchumi na Kidemokrasia pia.
Kwa Uchache tu, nakukumbushia Machache Miongoni Mwa Mengi aliyoyafanya:
• Arusha amepeleka Miradi Mkubwa wa Maji: Bilioni 520 Arusha Jiji, Mradi wa Maji Chanzo toka Mto Simba Kilimanjaro Bilioni 16, Ujenzi na Upanuzi wa Barabara Kuwa njia nne Kutoa Ngaramtoni hadi USA River ikiwemo zile za Mchepuko / Mzunguko ( By-Pass ) ambazo zimekamilika zaidi ya Bilioni 164, Tumejengewa Hospitali Mpya za Wilaya ya Longido ( Bilioni 2 ), H/Wilaya Karatu Bilioni 1.5, H/ Wilaya Ngorongoro ( Bilioni 1.8 ) na H/Wilaya Arusha ( Bilioni 1.5 ) Pamoja na Kuboresha Hospitali za zamani.
• Ununuzi wa Ndege Mpya 11 Kwa fedha zetu za ndani sio mkopo, yaani CASH PAYMENTS ( Boeing 787-8 Dreamliners ziko 2, Airbus 220-300 ziko 2, Bombadier Dash 8 Q-400 ziko 4 na nyingine Tatu kuja Miezi michache ijayo. Hapa Serikali ya Dkt. Magufuli imeboresha huduma ya Usafili wa Anga kupitia Shirika la Huduma ya Usafirishaji Kwa njia ya Anga Tanzania ( ATCL )ambapo Mapato yameongezeka na Utalii umeongezeka zaidi na Kuongeza Pato la Taifa.
• Ujenzi Mradi Mkubwa wa Uzalishaji Umeme wa Mwl. Nyerere - Megawati 2115 ( Stieglers Gorge ) utakaogharimu Pesa zetu za ndani Trilioni 6.5 ( Dola za Kimarekani Bilioni 2.9 ) hadi kukamilika Kwake na Kazi inaendelea vizuri sana.
• Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Treni ya Umeme ( SGR ) Kutoka Dar es salaam hadi Mwanza. Maendeleo ya Mradi wa Kipande cha Kutoka DSM-Morogoro na Kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma utagharimu Trilioni 7.062 fedha zetu wenyewe kwa kodi zetu. Kipande cha Mwanza –Isaka-Dodoma Maandalizi yanaendelea vizuri. .
• Rais Magufuli hakuwasahau wana Dar es salama. Kawapelekea Miradi ya Kutosha;
Miradi Mikubwa ya Ujenzi wa Madaraja na Barabara za Juu kama: Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu Ubungo ( Ubungo Interchange Flyover ( zaidi ya Bilioni 200 zimetumika ), Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu - Mfugale flyover ( zaidi ya Bilioni 247 ), Mradi wa Salender Brigde na Daraja la Majini Ziwa Viktoria Busisi – Kigongo urefu wa Km 3.2 litakalo gharimu Bilioni 699 pesa za Kitanzania hadi kukamilika kwake, ujenzi unaendelea vizuri sana.
• Mpango wa Elimu Bila Malipo Kuanzia Shule Msingi hadi Sekondari ambapo Serikali ya JPM inatenga zaidi ya Bilioni 23 Kila mwezi ili kugharamia Elimu Msingi hadi Sekondari.
• Rais Magufuli ametimiza ndoto ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. JK Nyerere ya Mpango wa Kuhamishia Serikali Dodoma. Dodoma sasa inapendeza, vijana wamepata ajira na Maendeleo Mkoa wa Dodoma sio suala la kuuliza Mwenye Majicho atizame mwenyewe.
• Mpango wa Kujenga Vituo vya Afya Kila Kata Nchini Kote Kwa Maeneo yasiyokuwa na Vituo vya Afya.
• Rais Magufuli pia ameweza Kujenga Hospitali Mpya za Wilaya Katika Halmashauri 67 Nchini Kote.
• Uboreshaji wa Viwanja vya Ndege ikiwemo Jengo Jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ( JNI ), Mradi uliogharimu Bilioni 722 Fedha zetu za ndani. Sambamba na hili tunakumbuka pia Ununuzi na Ujenzi wa Mifumo ya Kuongozea Ndege Katika Viwanja vya Ndege vya JNIA Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Songwe Kwa gharama ya Bilioni 67.3 Fedha zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli.
Ndugu zangu ni Mengi ya Kujivunia Kutokana na Uongozi wa Rais Magufuli. Nimeshindwa Kuyaandika yote maana ni Mengi sana.
Lakini hawa wengine , tujiulize wamefanya nini kwa taifa hili walipokuwa watumishi, au wabunge kumzidi JPM??
1. Wengine walipokuwa wabunge hawawezi kukuonesha hata mtaro wa maji waliosaidia kuujenga jimboni;
2. Wakiwa wabunge walisifika kwa kuzuia wananchi kushiriki maendeleo;
3. Wakiwa wabunge hawakuwahi kupitisha bajeti yoyote kwa maendeleo ya wananchi zaidi ya kuzikataa zote;
5. Kiongozi sahihi ni lazima Asisitize amani, Lakini wapo wagombea wengine hakuna mahali popote wamesisitiza amani zaidi ya vurugu.
6. Kiongozi Bora ni lazima awe mzalendo wa taifa lake...Lakini wapo wengine Wanaonekana kuamini katika mataifa ya nje kuja kuwasaidia kwa kufikiri na kutekeleza.
7. Wapo waonaponda kila kitu cha nchi wakiwemo Waasisi wa Taifa
8. Wapo waonaponda kila maendeleo yaliyopo nchini ikiwemo barabara wanazopita, maji wanayokunywa, umeme wanaoutumia kila siku n.k
By Mpekuzi
Post a Comment