Mchekeshaji wa Miaka 19 Kenya Apewa Mkataba na Rihanna |Shamteeblog.


Mchekeshaji Elsa Majimbo ambaye amejipatia umaarufu kwa hotuba zake katika mtandao wa twitter na Instagram tangu kuanza kwa mlipuko wa Corona amefanikiwa kuingia mkataba na nembo ya fasheni ya Rihanna kwa jina Fenty.


Mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alisema kwamba anajivunia mkataba wake wa kukuza nembo hiyo ya Rihanna. Nembo hiyo ya Rihanna ilituma ujumbe kwa njia ya video katika mtandao wa twitter ambapo ilitangaza mpango huo.


”Naishukuru familia ya fenty wamekuwa watu wazuri pamoja na Rihanna katika nembo hii”, Elsa alituma ujumbe wa twitter.

“>Video zake za vichekesho alizopiga chumbani akiegemea mto huku akiwa anakula vipande vya ‘klipsi’ wakati akiwa anazungumza zimewavutia watazamaji wengi barani Afrika .

“>Mwezi Julai, aliambia gazeti la Uingereza The Guradian kwamba familia yake haipendi video zake lakini sasa wameanza kuzipenda polepole. Alisema kwamba katika siku za baadaye atafanya uigizaji na kusoma kidogo – ni mwandishi katika Chuo Kikuu cha Strathmore jijini Nairobi.

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post