Wataalam wa Tehama kusajiliwa rasmi |Shamteeblog.

WATAALAM wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA), wanatarajiwa kuanza kusajiliwa rasmi katika kongamano la nne la mwaka linalotarajia kufanyika kati ya Oktoba 7 hadi 9 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu, Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dk.Zainab Chaula alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo.

Amesema hatua hiyo ni katika kutekeleza sera ya taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 inayotaka kuwa na nguvu kazi yenye maadili na uwezo wa hali ya juu katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na kukuza mchango wake katika maendeleo ya nchini.

“Kwa kipindi kirefu tumekuwa na wataalamu wanaosimamia miundombinu, huduma na mifumo yetu muhimu ya TEHAMA pasipo kutambulika uwezo na maadili yao, hivyo katika kongamano la mwaka huu, moja ya tukio muhimu ni kuzindua rasmi usajili wa wataalam wabobezi wa TEHAMA na waziri mwenye tamana ya TEHAMA atatoa vyeti vya usajili kwa wataalam 100,”amesema.

Aidha, Dk. Chaula amesema mijadala katika kongamano hilo lenye kaulimbiu ‘kuelekea mapinduzi ya nne ya viwanda: kinachofanyika, changamoto na fursa’.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post