Kocha Mkuu Mpya wa Yanga Cedric Kaze Raia wa Burundi amewasili Tanzania akitokea Canada.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini Kocha huyo amesema kuwa anaimani atafanya kazi vizuri na klabu hiyo kwani ni klabu kubwa na yenye mashabiki wengi barani Afrika na kuwataka mashabiki kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kupata mafanikio.
“Na wafans wetu wajiandae kabisa wasapoti timu tushirikiane najua kama tutafanya vitu vikubwa” Amesema Kaze
Kocha huyo wa zamani wa vilabu kama Vital O na Altletico Fc anakuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mserbia Zlatko Krmpotic aliyevunja mkataba na klabu hiyo mapema mwezi huu baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union uliomalizika kwa Yanga kushinda Goli 3 kwa sifuri.
Hata hivyo Klabu ya Yanga ilimalizana na Mburundi Cerdric Kanze lakini baadae alishindwa kuwasili nchini. Ndipo ikawalazimu kumpata Mserbia Zlatko Krmpotic ili aweze kuchukua nafasi hiyo.
Cedric Kaze ni kocha Raia wa Burundi mwenye leseni ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CUF) pamoja na shirikisho la soka nchini Ujerumani (DFB)
Yanga ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na point 13 na kucheza mechi 5. Cedric Kanze ambaye ni kocha bora nchini Burundi kwa msimu wa mwaka 2011/2012 atakuwa na kibarua cha kukiongoza kikosi cha wananchi katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara siku ya tar 22 october dhidi ya Polisi Tanzania.
By Mpekuzi
Post a Comment