TAMWA yaomba wazazi na walezi kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike |Shamteeblog.

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), kimeiomba wazazi na walezi kutoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia wanazofanyiwa watoto wa kike nchini.

Akizungumzia siku ya mtoto wa kike Duniani, Mwenyekiti wa chama hicho Joyce Shebe amesema kuwa wazazi na walezi wanawajibika kutoa taarifa kuhusu matukio hayo kwani kuna taasisi mbalimbali zenye uwezo wa kushughulika nayo kwa lengo la kujenga kizazi bora cha baadae.

“TAMWA tunaomba wazazi, walezi na watoto wa kike,wanaofanyiwa ukatili, wavunje ukimya, kwani zipo asasi, taasisi na vyombo vya serikali ambavyo wanaweza kuvitumia kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia Amesema shebe

Joyce Shebe ameongeza kuwa serikali inapaswa kuandaa utaratibu wa ulinzi, utoaji taarifa na ufuatiliaji kwa watoto hasa wakati wa dharura za milipuko ya magonjwa au majanga kama Covid-19 ili kuepusha madhara yanayoweza kuzuilika.

Katika hatua nyingine Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini (TAMWA) kimeendelea kukumbusha umuhimu wa mabadiliko ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kueleza kuwa mtoto wa kike mwenye umri chini ya miaka 18, bado hajapevuka vya kutosha kumudu majukumu ya ndoa na kubeba ujauzito na kuhimiza umuhimu wa kutoae elimu kwa mtoto wa kike na kumpa fursa ya kusikilizwa sawa na mtoto wa kiume

Chama hicho kimeipongeza serikali, chini ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa jitihada za ulinzi na afya kwa watoto wa kike, huku kikisisitiza ulinzi kwa mtoto wa kike kupitia kauli mbiu ya Mtoto wa mwenzio, ni wako, mlinde pamoja na kaulimbiu ya siku ya mtoto wa kike duniani isemayo Sauti yangu, ni mustakabali wetu wa usawa.

Siku ya mtoto wakike duniani huadhimishwa kila siku ya tar 11 mwezi oktoba kila mwaka ambapo nchini Tanzania maadhimisho yanaongozwa na kauli mbiu inayosema Tumuwezeshe mtoto wa kike, kujenga taifa lenye usawa wakati kauli mbiu ya kitaifa ikiwa inasem Sauti yangu, ni mustakabali wetu wa usawa.’



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post