Watazania laki sita hawaoni – Dk. Magembe |Shamteeblog.

Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Grace Maghembe,amesema inakadiriwa kuwa watanzania laki sita hawaoni huku akitoa wito kwa wananchi kuepuka kutumia dawa ya macho kiholela bila ya kuwa na maelekezo kutoka kwa Daktari.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuadhimisha siku ya Afya ya macho Duniani Dkt.Maghembe amesema kuwa ni muhimu mtu kufika hospitalini mara tu anapoona kuwa ana matatizo ya macho na sio kutumia dawa ambazo sio rasmi kwa ajili ya matibabu .

Dkt Maghembe amesema inakadiriwa kuwa watanzania 600,000 hawaoni huku watu wenye matatizo ya kuona kwa kiwango cha kati na cha juu hapa nchini wanakadiriwa kuwa ni mara tatu ya watu wasioona ambao ni takriban milioni 1.8 hivyo kwa ujumla Tanzania ina watu milioni 24 wenye matatizo ya kuona .

“Watu milioni 24 sawa na asilimia 2.5 ya watanzania wote wana ulemavu wa kutokuona ikijumuisha na upungufu wa kuona na asilimia kubwa ya matatizo haya yanasababishwa na upungufu wa kuona unaorekebishika kwa miwani 45%,mtoto wa jicho 28.8%,shinikizo la jicho 8%, kovu kwenye kioo cha mbele cha jicho na Trakoma 5%, athari ya ugonjwa wa kisukari kwenye pazia la jicho na matatizo ya pazia la jicho kwa watu wazima 4%,matatizo ya kutokuona utotoni 2%,na Mengineyo 8.2%”amesema Dkt.Maghembe.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post