Na MWANDISHI WETU
BENKI ya Azania ikiwa katika maadhimisho ya kusherekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwake, leo imezindua huduma mpya ya kisasa ya kadi za aina mbili za Visa kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
Kadi hizo za aina mbili, ambayo ni kadi za kawaida (Classic) na zile za daraja la juu (Infinite) ambazo itatumiwa na wateja wake wa akaunti maalumu, zimezinduliwa katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo zilizopo Obama Drive, Sea View-Upanga jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Novemba 25, katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Charles Itembe amesema
kwa kutumia kadi hizo mbili sasa wateja wa benki hiyo wataweza kufanya miamala popote duniani na kuweza kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao, kufanya malipo kwa kutumia kadi hizo za Visa kwenye maduka mbalimbali.
Amesema wateja wa kadi za daraja la juu (Infinite card), wataweza kupata huduma za ziada ikiwamo huduma katika viwanja vya ndege, hoteli za kimataifa na kadhalika.
Itembe ameshukuru bodi ya benki hiyo kwa kuwaunga mkono katika kufanikisha safari ya benki hiyo yenye lengo la kuifanya kuwa ya kisasa zaidi.
“Ikumbukwe kuwa kipindi hiki tuko katika maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki yetu mwaka 1995, kwa kuwajali wateja wetu kwa kutuunga mkono kwa miaka 25 tumehakikisha wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma zetu zote zikiwamo za kubenki kidijitali, kwa kutumia simu zao za kiganjani kwa mobile App iliyoboreshwa.
“Mawakala wetu ambao wamesambaa nchi nzima, matawi yetu ambayo sasa yamefikia 24 ambapo baadhi yanatoa huduma 8-8, siku zote saba za wiki, vituo vyetu vya kutolea huduma (Service Centres), maduka ya kubadilishia fedha yanayojitegemea 12.
“Na mwishoni mwa wiki hii pia tunakwenda kufungua duka jingine la 13 katika uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA Terminal III), na huduma nyinginezo nyingi na za kipekee kabisa. Na sasa tumewaletea huduma hii kubwa kabisa ya kadi za VISA.
“Benki yetu imewekeza katika teknolojia ya kisasa, mfumo wetu wa teknolojia ya kibenki wa Oracle Flexcube toleo la 12.4 ni wa kisasa zaidi na ndio uliotuwezesha kutuunganisha na huduma hii ya VISA inayopatikana dunia nzima na wateja wetu sasa wataweza kupata huduma kwa kutumia kadi zao za VISA popote duniani,”amesema.
Naye, Meneja wa huduma za Benki Kidijitali wa benki hiyo, Vinesh Davda amesema huduma hiyo itawapa urahisi wateja wa benki huku akiwaomba wateja kutembelea matawi ya benki hiyo ili kuweza kupata kadi hizo mpya.

from Author
Post a Comment