Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi Waziri wa Ulinzi Mark Esper kuashiria kuwa huenda akatumia miezi yake ya mwisho madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi kufanya maamuzi ya kulipiza kisasi katika serikali yake.
Trump alikuwa amezozana na Esper kuhusu msururu wa masuala na alikasirishwa hasa na hatua yake ya kupinga hadharani vitisho vya Trump vya matumizi ya wanajeshi katika kupambana na maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi baada ya polisi kumuua George Floyd mjini Minneapolis.
Trump alisema kwenye Twitter kuwa Christopher Miller, mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa Kupambana na Ugaidi, anachukua usukani kama kaimu waziri wa ulinzi.
Miller, mwenye umri wa miaka 55, amekuwa mkurugenzi wa kituo hicho tangu Agosti. Ni mwanajeshi wa zamani aliyehudumu jeshini kwa miaka 31.
By Mpekuzi
Post a Comment