Lissu, Mbowe mbaroni |Shamteeblog.

Mwandishi Wetu, Dar es salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema linawashikilia baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa tuhuma za kuratibu maandamano.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alieleza kuwa licha ya viongozi hao kusema kuwa maandamano hayo ni ya amani, lakini wamebaini uwepo wa vitendo vya uvunjifu wa amani na uharibufu wa mali za wananchi.

Aliwataja viongozi wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Freeman Mbowe, Godbless Lema na Boniface Jacob.

“Kama ilivyotokea Oktoba 29 na 30 nilitoa taarifa kwa umma kwamba tumesikia fununu kuwa kuna watu ambao wamesema hawakubalini na matokeo ya uchaguzi na kwamba wanapanga kuingia mitaani kufanya vurugu kama sehemu ya kuonesha kuwa hawakubaliani na maamuzi ya wananchi.

“Tulitoa katazo kwamba kitendo hicho hakikubaliki. Suala la kuingia kwenye ushindani wa kutafuta ridhaa ua kuchaguzliwa lilianza kwa kuuza sera, ni masuala sasa ya kuacha mikononi mwa wananchi wenyenyewe ndio waamue kiongozi gani anayewafaa.

“Na tumepiga marufuku maandamano hayo lakini wote walioshindwa mikoani huko sasa wanajikusanya Dar es Salaam na wanachokifanya sasa ni kutangaza kuratibu na kusimamia maandamano ambayo tuliyakataza, kwamba yangefanyika kuanzia asubuhi ya jana.

“Na walichokifanya wamekuwa wakifanya vikao mbalimbali ambavyo kwa kupitia watu wetu wa taarifa fiche wamekuwa wakiendelea kuwapa taarifa za namna wanavyoendeela kupanga na kuratibu maandamano hayo, lakini kibaya zaidi ni kwamba maandamano hayo yaliambatana na maelekezo yaliyotolewa kwa watu walioshawishika kwamba pamoja na kuandamana, wangeendelea kufanya uharibifu wa miundombinu, walipanga kuchoma masoko, lakini pia walipanga kuchoma vituo vya mafuta na walipanga kuchoma magari ambayo wangekutana nayo wananchi wakienda kazini au wakitoka kazini kwenda majumbani,” alisema.

Alisem akutokana na mpango huo walitarajia kufanya fujo kubwa ambayo walikuwa wameipanga, ambapo wamekusanya viongozi mbalimbali kutoka katika maeneo yote wakiwemo akina Joseph Mbilinyi (Sugu), Lema na wengine ambao wamekuja kwa ajili ya kufanya oparesheni hizo.

Alisema wameshawakamata baadhi ya wengine na kwa sasa oparesheni kubwa inaendelea na yeyote anayeshiriki kuratibu, kuendesha au kuingi barabarani atakutana na mkono wa sheria.

“Nilisema hilo tayari Mbowe, Lema na Jacob tumeshawakamata, tunao na kijana ambaye ni tunda la kushawishiwa tayari tunaye hapa na oparesheni inaendelea, wote wanaohusika watakanatwa na wanaendelea kuhojiwa na mwisho ni kukamilisha utaratibu wa kuandaa jalada kwa ajili ya kwenda mahakamani,” alisema Kamanda Mambosasa.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post