Magufuli: Vitambulisho vya wajasiriamali Vitaboreshwa |Shamteeblog.


Rais Magufuli   amesema, vitambulisho vya wajasiriamali ‘machinga’ vitaboreshwa zaidi ili kuwawezesha kupata mikopo benki.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akihutubia na kuzindua Bunge la 12 leo Ijumaa tarehe 13 Novemba 2020 jijini Dodoma.
 

Amesema, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, vitambulisho vya wajasirimali vilivyokuwa vinatolewa huko nyuma sasa vitaboreshwa zaidi kwa kuweka taarifa muhimu.

“Kwa miaka mitano ijayo, tutaviboresha ikiwemo kuweka picha na taarifa nyingine muhimu kama ilivyo kwenye vitambulisho vya taifa na paspoti.

“Hii itawezesha wafanyabiashara watakaotumia vitambulisho hivyo kutambulika ikiwemo kwenye benki na hivyo kupata mikopo ili kukuza biashara zao,” amesema Rais Magufuli

Amesema, hatua hiyo “itawawezesha kukuwa na kutajirika, tunataka wafanyabiashara wadogo wadogo kukuwa na siyo kubaki walivyo”



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post