”Mimi ni Tanzania One” Mwakinyo Atamba |Shamtee.blog

Bondia Hassan Mwakinyo amesema yeye ndie bondia namba moja nchini baada ya kumchapa Muajentina Jose Carlos Pazi katika pambano lililofanyika katika ukumbi wa ndani wa Next Door Masaki Dar es salaam.

Kwa ushindi wa Tko aliopata katika raundi ya nne,Mwakinyo amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa WBF Intercontinental Super Welterweight.

“Nilikuwa nimejipanga kushinda na ninafurahi kushinda katika hili huu ni ushindi wa Tanzania kiujumla, mashabiki pamoja na Serikali ambayo inanipa sapoti,” alisema Mwakinyo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari.

The post ”Mimi ni Tanzania One” Mwakinyo Atamba appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post