Mo Ibrahim aziumbua nchi za Afrika |Shamteeblog.

ADDIS ABABA, ETHIOPIA

RIPOTI kuu iliyotolewa juzi Jumatatu inaeleza kuwa, mchakato wa utawala bora umedorora barani Afrika kwa mara ya kwanza katika kipindi cha muongo mmoja hata kabla ya maambukizi ya corona kuiathri dunia huku masuala ya kuheshimu demokrasia na haki za binadamu yakidorora.

Ripoti inayotolewa na Taasisi ya Mo Ibrahim ambayo huchapishwa kila baada ya miaka miwili huipatia kila nchi maksi za utendaji kwa mujibu wa vigezo zikiwemo hatua za kupambana na ufisadi, kulinda haki za raia na kulinda mazingira. 

Ripoti hiyo imeeleza kuwa, zaidi ya asilimia 60 ya Waafrika wanaishi katika nchi ambazo zimepiga hatua katika utawala bora katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2019. 

Taasisi ya Mo Ibrahim imeongeza kuwa, hata hivyo mafanikio yamepungua katika miaka mitano ya karibuni; na mwaka huu kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 10 maksi za pamoja kwa nchi zote zimeshuka kutoka mwaka hadi mwaka.

Taasisi hiyo iliundwa mwaka 2006 kujikita katika suala la kuwepo haja ya uongozi bora wa kisaisa na utawala bora barani Afrika kwa kuzingatia kuongezeka ukandamizaji ambapo watu wanashindwa kutumia haki yao ya kidemokrasia na kushiriki katika asasi za kiraia. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, mazingira hatarishi kwa haki za binadamu yamekuwa yakiongezeka siku baada ya siku na pia kudorora kwa hali ya usalama. 

AP



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post