Simba Sc Wamuita Chama Mezani |Shamtee.blog

Klabu ya Simba sc ipo mezani na kiungo Cletous Chama kuzungumza kuhusu kuongeza makataba na klabu hiyo kwa muda wa miaka miwili zaidi taarifa zinadai.

Kiungo huyo ambaye mkataba wake na klabu hiyo unaisha mwishoni mwa msimu huu amewatia hofu wanachama na mashabiki wa klabu hiyo juu ya mstakabali wake klabuni hapo baada ya taarifa kuzagaa kuwa ananyemelewa na klabu ya Yanga sc pamoja na klabu za nje ya Tanzania.

Mpaka sasa inadaiwa klabu hiyo imemuwekea kiungo huyo fedha zinakadiriwa kufikia milioni 250 pamoja na mshahara wa milioni 15 kwa mwezi huku wakishinikiza asaini mkataba wiki hii.

The post Simba Sc Wamuita Chama Mezani appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post