Waathirika dawa za kulevya waomba elimu wakipokea msaada wa Meridian Bet |Shamteeblog.

Mwandishi Wetu

Waathirika wa dawa za kulevya wanaotibiwa kwenye kituo cha Pedderef kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam, wameomba jamii ipewe elimu ya kutowanyanyapaa na kuwaona kama watu wasioaminika.

Waathirika hao wametoa kauli hiyo jana wakati wakipokea msaada wa vyakula na mahitaji mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya kubashiri ya Meridian Bet.

Mmiliki wa kituo hicho, Nuru Salehe ambaye amekiri kuwahi kuwa muathirika wa dawa za kulevya kwa miaka 12 kabla ya kuacha miaka tisa iliyopita, alisema waathirika wa dawa hizo wamekuwa wakikutana na changamoto ya kunyanyapaliwa hata baada ya kutoka soba.

“Jamii inapaswa kupewa elimu juu ya tatizo hili, ni ugonjwa kama yalivyo magonjwa mengine, lakini kuna changamoto muathirika anapoamua kuacha na kuomba aidha kurudi shule au kupewa biashara afanye jamii nyingi zinakuwa hazina imani naye.

“Changamoto hii inapelekea wengine kujikuta wakirudia kutumia dawa wakiamini watapata faraja hivyo badala ya kutatua tatizo wanaliongeza,” alisema.

Akikabidhi msaada kwenye kituo hicho, meneja mafunzo wa Meridian Bet, Sadick Mhema alisema, kampuni yao imeamua kuwashika mkono wa faraja waathirika hao wa dawa za kulevya ili kama sehemu ya mkakati wa kampuni kurudisha kwa jamii.

“Tumetoa vyakula mbalimbali na vitu vingine vya mahitaji ya kibinadamu kwenye kituo hiki kama mpango wa Meridian Bet katika kurudisha kwa jamii,” alisema Mhena wakati wa kukabidhi msaada huo akiwa sanjari na watumishi wengine wa Meridian Bet na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Chetan Chudasama.

Alisema wamekuwa wakitoa misaada kama hiyo katika maeneo mbalimbali yenye jamii yenye uhitaji ikiwamo kituo cha wazee Tabata na kwa wagonjwa wa kansa wanaotibiwa Hospitali ya Ocean Road Dar es Salaam.

“Kampuni ya Meridian Bet tuna utaratibu wa kusaidia jamii yenye uhitaji, leo tumeamua kuwashika mkono wa faraja wenzetu wa soba ya Pedderef kama moja ya malengo ya kampuni kwa kurudisha kwa jamii,” alisema.

Mmiliki wa kitu hicho, Nuru Salehe aliwashukuru Meridian Bet kwa kujitoa huko na kusema ni kamouni ambayo imeonyesha mfano kwa kujitoa kuwasaidia.

Meneja wa kituo hicho, Juma Kwame alisema kituo kina zaidi ya waathirika 40 ambao wanatibiwa kwa kupatiwa ushauri.

“Wanapofika kituoni siku ya kwanza wanaangaliwa na dakatrai na kupewa dawa ya kuondoa ‘alosto’ kwa siku saba baada ya hapo wanaanza kutibiwa kwa kupewa ushauri na kujifunza masuala ya kimaiasha, program inayofanyika kwa mwaka mmoja na wapo wanaoacha,” alisema.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post