Yanga Sc Yaishusha Azam Fc |Shamtee.blog

Bao la Deus Kaseke dakika ya 49 lilisababisha Yanga sc ipande mpaka kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kunyakua alama tatu mbele ya Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

Awali Yanga sc ilikua na alama 25 sawa na Azam Fc lakini utofauti katika uwiano wa magoli ya kufungwa na kufunga ulisababisha Azam fc kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Kuumia kwa mshambuliaji Prince Dube dakika ya 18 kulipoozesha mashambulizi ya Azam Fc ambao mpaka mpira unaisha walikua hawajalenga lango la Yanga sc.

Hii ni mechi ya pili mfululizo kwa Azam Fc kupoteza mchezo wa ligi kuu baada ya kufungwa bao 1-0 na Kmc katika mchezo wa raundi  iliyopita.

The post Yanga Sc Yaishusha Azam Fc appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post