Yanga sc Yateua Mrithi wa Katibu Mkuu |Shamtee.blog

Uongozi wa Klabu ya Yanga sc leo umemtangaza Mkurugenzi wa fedha wa klabu hiyo  CPA Haji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu akuchukua nafasi ya Wakili Simon Patrick aliesimamishwa.

Baada ya kutangazwa Mfikirwa ameushukuru Uongozi wa Klabu hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo ambayo imekua ni mwiba mkali kwa wanaoteuliwa tangu ajiuzuru Boniface Mkwasa.

Amesema kikubwa kilichopo kwa sasa ni kuhakikisha anasimamia na kufanikisha mipango yote ya Klabu iliyopo.
Mipango hiyo ni ubingwa, mabadiliko ya uendeshaji wa Klabu na ujenzi wa Hostel na Uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo Kigamboni.
.

The post Yanga sc Yateua Mrithi wa Katibu Mkuu appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post