Picha haihusiani na habari hapa chini
Na Anthony Mayunga - Mwananchi
Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara wanamshikilia Juma Masiaga (38) mkazi wa kijiji cha Kitunguruma kwa tuhuma ya kumchinja kaka yake, Chacha (40) kwa madai ya kutomlipa Sh700,000/=.
Akizungumza na Mwananchi Digital jana Alhamisi Desemba 24, 2020 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema tukio hilo limetokea jana saa nne usiku.
"Alimvizia na kumkata shingoni na kichwani kisha akakimbia na leo amenaswa eneo la jalala kuu mjini Mugumu akijaribu kutoroka, sasa anahojiwa na polisi kwa ajili ya hatua zaidi," amesema.
Amesema taarifa zilizopo ni kuwa alikuwa akimdai kaka yake Sh700,000/= baada ya awali kulipwa Sh800,000/=.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Joseph Petro amesema hakuwahi kusikia mgogoro wowote wa ndugu hao na kwamba kama alikuwa na malalamiko angeyawasilisha sehemu husika.
By Mpekuzi
Post a Comment