FAO yaanza na halmashauri 3 kujenga uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa. |Shamteeblog.


Ofisiya Waziri Mkuu kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa kushirikiana na Shirika laChakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),wameanza kuwajenge au wezo wadau wa Afya moja na wataalam kutoka sekta za afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo, kilimo na mazingira, juu ya namna ya kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa ambao umekuwa ni tishio la ustawi wa Afya na uchumi.

Kufuatia nchi ya Tanzania kuwa imepiga hatua katika uratibu wa masuala yaAfya moja, ambayo ni dhana inayo jumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo, kilimo na mazingira kushirikiana kwa pamoja katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. FAO imeanza kutumia dhana hiyo kwakuwa inapunguza gharama katika kushughulikia athari za usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya Dawa.

Usugu wa vimelea vya magonjwa ni hali ya dawa kushindwa kudhibiti vimelea vya magonjwa kwa kushindwa kabisa kuviua au kuzuia ukuaji wa vimelea hivyo. Vimelea ambavyo vinakuwa sugu dhidi ya dawa vinajumuisha bakteria, virusi, fangasi, na “parasite”. Hali hii hupelekea dawa kushindwa kufanya kazi na kutoa matokeo yanayotarajiwa.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo, mjini Morogoro, Mratibu Taifa, Dawati la  Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka amebainisha kuwa ushirikiano wa wadau wa Afyamoja na wataalam na sekta za Afya  kwakutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima, ambapo wadau wa afya moja wanawajibika kupanga mikakati mbalimbali ya kupambana na usugu wa vimelea vya mogonjwa dhidi yadawa.

“Moja ya mkakati ulioibuliwa Kitaifa na Kimataifa ni kujiandaa kwa kuwa fundisha wataalam wa sekta za afya na wadau wa Afya moja jinsi ya kuwa na kufanya tathmini ya hatari ya vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa kwa ushirikiano.” Amesema Chinyuka.”

Kwa upande wake, Mratibu  wa Mafunzo hayo kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), Tanzania, Elibariki Mwakapeje, amefafanua kuwa Shirika hilo moja ya kipaumbele chake ni kupambana na Usugu wa kupunguza umasikini na kuongeza kipato cha wananchi, hivyo Shirika hilo linashirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, katika kujenga uwezo wa  ndani ya nchi kwa kuwafundisha wataalam wa sekta za Afya katika kudhibiti magonjwa ambapo uwezo huo utasaidia kuimarisha afya ya binadamu na mifugo na hatimaye kipato kitaongezeka na umasikini utapungua

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamebainisha kuwa wamepata uwezo wa kujenga mtandao wa Afya moja kwenye halmashauri ambao utaweza kupambana na sababu zinazo sababisha usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa ambazo ni; Kutumia dawa bila ushauri wa kitaalamu katika sekta zote za afya ya binadamu,mifugo na mimea. Kutokamilisha dozi sahihi ya dawa, Kutozingatia kanuni sahihi za usafi kama unawaji wa mikono pamoja na matumizi holela ya dawa zinazopaswa kutumika baada ya vipimo na ushauri wa daktari/mfamasia au wataalamu wengine wa afya waliothibitishwa.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisiya Waziri Mkuu, kupitia Dawati hilo kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) waliandaa na kuratibu mafunzo hayo, ambapo wataalamu wa sekta za Afya na Wadau wa Afya moja kutoka Halmashauri tatu kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Mwanza kwa Halmasahauri yajiji la Arusha na Halmasahauri ya Manispaa ya Temeke na Halmashauri yaManispaa ya Nyamaga.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post