NI miaka saba imepita tangu Alex Ferguson alipoipa kisogo Manchester United na tangu kipindi hicho timu hiyo imeshindwa kuwa kwenye ubora wake wa miaka mingi iliyopita.
Je, ‘babu’ huyo mwenye umri wa miaka 78 amewahi kuwazungumziaje David Moyes, Louis van Gaal, Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer waliojaribu kuziba pengo lake? David Moyes (Mechi 51, akashinda 27)
“Tulimchagua David Moyes. Alikuwa na mwendelezo mzuri akiwa na Everton na alidumu kwa muda mrefu, miaka 11… Kwa bahati mbaya, mambo hayakuwa mazuri kwa David, ingawa hakufanya vibaya.
“Nafikiri angefanikiwa kama angepata nafasi nyingine Old Trafford.”
Louis van Gaal (Mechi 54, akashinda 103)
“Louis van Gaal alifanya mabadiliko mengi sana na lilikuwa jambo zuri kujenga timu upya kwa sababu ana uzoefu na uwezo mzuri wa kufanya hivyo.”
Jose Mourinho (Mechi 144, akashinda 84)
“[Mourinho] ametwaa mara mbili mataji ya Ulaya, amebeba ubingwa wa ligi katika kila nchi aliyokwenda, amenyakua vikombe vingi vikubwa…”
Ole Gunnar Solskjaer (Mechi 110, akashinda 61)
“Amekuwa mtumishi mzuri kwa klabu na mara zote ni mfano wa wachezaji kwa alivyokuwa akijituma uwanjani. Pasi na shaka, Ole atakuwa kocha mkubwa.”
from Author
Post a Comment