OWA, Marekani
MWIMBAJI nyota wa Injili pande za Chicago, Marekani, Maisha Manasse, amesema wimbo wake mpya, Muweza, umebeba ushuhuda wa maisha ya kweli aliyowahi kuishi kabla ya kufanikiwa alipofika sasa.
Manasse, amesema wimbo huo unaotarajia kutoka December, 31, mwaka huu utabadilisha maisha ya watu wengi katika kumtegemea Mungu kwenye kila magumu wanayopitia kama ambavyo yeye alimtegemea na akamvusha kwenye changamoto nyingi.
“Nashukuru Mungu wimbo umekamilika na video itatoka mwishoni mwa mwaka huu. Naishukuru timu yangu ya hapa Chicago na Iowa kuanzia meneja wangu, Danny Dee Fodi ambaye aliandika script ya video yote na kubuni mavazi niliyovaa pia dada Scola na kaka Godwin ambao waliingiza ndani ya video na bila kumsahau director Dieudonne Nb ambaye anafanya vizuri sana hapa Marekani, mashabiki watarajie kubarikiwa na kuongeza viwango vyao vya imani kupitia video hiyo ambayo itakuwa kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema Maisha mwana wa Manasse.
from Author
Post a Comment