Nyota Yanga Aandaliwa Mapokezi Kabambe |Shamtee.blog

Mshambuliaji Saido Ntibanzokiza aliyesajiliwa na Yanga sc kwa usajili wa dirisha dogo anatarajiwa kuwasili nchini muda wowote kuanzia sasa huku akiwa ameandaliwa mapokezi kabambe unaambiwa.

Inadaiwa klabu hiyo imeandaa utaratibu maalumu wa mapokezi ambapo jumla ya jezi 500 originali zenye jina la mchezaji huyo zimeandaliwa kwa ajili ya mapokezi na zitauzwa kwa bei ya Tsh 35000.

Klabu ya Yanga sc ilimsajili kiungo huyo alipokuja kuitumikia timu ya Taifa ya Burundi katika mchezo wa kirafiki na kufanikiwa kufunga bao 1 lililoipa alama timu yake ndipo Yanga sc ilipomuwahi na kumsajili lakini ilimpasa kusubiri mpaka wakati wa dirisha dogo ili usajili wake uidhinishwe.

The post Nyota Yanga Aandaliwa Mapokezi Kabambe appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post