Rose Muhando atwaa tuzo Burundi |Shamteeblog.

Na CHRISTOPHER MSEKENA

MIAMBA imeendelea kupasuka baada ya Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania, kutunukiwa tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika Mashariki kwenye tamasha la Edge Festival lililofanyika jana huko Siege Social International nchini Burundi.

Rose ambaye kwa sasa amerudi kivingine na kufanikiwa kutikisa chati za muziki huo kwa wimbo wake mpya, Miamba Imepasuka, amesema anamshukuru Mungu kwa kuendelea kumpa kibali cha huduma yake kukubalika na kuendelea kupata mialiko mbalimbali licha ya kupitia changamoto nyingi.

“Leo nimepokea tuzo kubwa sana, tupo wengi hii ni neema si kawaida, Mungu ameendelea kuthamini kazi yangu ndio maana nimeendelea kupata mialiko mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwa ni miaka mitano imepita bila kutoa wimbo, nimetoa wimbo mpya uliobeba ushuhuda wa maisha yangu unaitwa Miamba Imepasuka na pia umebeba jina la albamu yangu ambayo itatoka Januari 8, 2021, hivyo wapendwa wajiandae,” alisema Rose.

Mwimbaji huyo ambaye ana miaka 16 kwenye huduma ya uimbaji anatajwa kama muimbaji aliyeuza zaidi nakala za albamu zake ambazo ni Mteule Uwe Macho (2004), Kitimutimu (2005), Jipange Sawa Sawa (2008), Nyota ya Ajabu (2010), Utamu wa Yesu (2011), Nampenda Yesu (2017), Usife Moyo (2018).



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post