Saido Amfurahisha Kaze |Shamtee.blog

Kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefurahishwa na kiwango cha mchezaji wake mpya Saido Ntibazonkiza alichokionyesha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United.

Kaze aliyemsajili mchezaji huyo ukiwa na usajili wake wa kwanza amesema kiwango alichokionyesha mchezaji wake anakifurahia kwani ameongeza kitu katika timu yake.

“Saido ni mchezaji mzuri na ameongeza kitu kwenye kikosi, ni mchezaji kiongozi na ameongoza vyema wachezaji wenzake”.

Saido alicheza mchezo wake wa kwanza katika mchezo huo na kufanikiwa kufunga mabao mawili huku akitoa pasi za kufunga zaidi ya tano lakini umakini mdogo wa Waziri Junior na Ditram Nchimbi ulisababisha kukosa mabao ya wazi.

The post Saido Amfurahisha Kaze appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post