WANANCHI RUANGWA WAPOKEA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA |Shamteeblog.

 

Kulia ni Mhandisi Senzia Maeda Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliagi akionesha Hati ya kukamilika kwa kazi ya Ujenzi wa Mradi wa Nanganga kwa Uongozi wa Halmashauri ya Ruangwa, wajumbe na baadi ya wananchi hawapo katika picha, kushoto ni Bw. Ramadhan Mwitage mwakilishi kutoka kampuni ya Haricom International Ldt ya Dar es Salaam Iliyofanya kazi ya ujenzi.
Picha ikionesha banio ni moja ya miundombinu katika skimu ya Kilimo cha  Umwagiliaji Nanganga.
kulia Bw. Nuru Chande Makamo mwenyekiti wa kamati ya wananchi ya ujenzi wa mradi kutoka kijiji cha Nanganga akionesha Hati ya kukamilika kwa mradi, kushoto ni Bw. Saidi Nchia mwenyekiti wa kamati hiyo.
Picha ikionesha mfereji mkuu unaochukua maji kutoka kwenye chanzo cha maji cha mto Lukuledi na kupeleka mashambani


 Na; Mwandishi Wetu–Ruangwa


Wananchi wa Kijiji cha Nanganga kilichopokatika kata ya Nanganga Wilayani Ruanga MkoaniLindi, wamepokeamradiwakilimo cha Umwagiliaji, wenye thamani ya kaisi cha fedha zaidi ya shilingi Bilioni Moja, Uliojengwa na Serikali ya Awamu ya tano,kupitia Wizara ya Kilimo chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kushirikiana na Halmashauri ya Ruangwa na fedha za ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).


Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho baada ya makabidhiano ya mradi huo, Diwani wa kata hiyo Shabani Kambona alisema wamepokea mradi huo wenye jumla ya hekta 300 za umwagiliaji ambapo ujenzi wa mradi huo kwa awamu hii utawezesha hekta 120 kumwagiliwa .

 “Ninaishukuru Serikali yetu pendwa kwa kuleta mradi huu na ninaimani kubwa sana kwa wana Ruangwa kuwa sasa ni wakati wa wao kujikita zaidi katika kilimo biashara na kuweza kupata chakula kutoka hapa hapa Raungwa bila kuagiza nje ya Mkoa wetu, na kuongeza pato la taifa na pato la mwananchi mmojamoja.” Alisema


Aliendelea kusema kuwa Skimu hiyo itaweza kuwasaidia wananchi Wilayani humo kulima mazao ya chakula na mboga mboga na kuwa na uhakika wa chakula.


Kwa upande Mwingine pamoja na kupokea mradi huo, Diwani kambona aliiomba Serikali kumalizia kusakafia mfereji wa upili wenye urefu wa mita elfu mbili (2000) ili kupunguza upotevu wa maji kwenye mifereji pamoja na kuchimba mitaro nane (8) yakutolea maji mashambani.

Mradi wa Nanganga ni kati ya Miradi kumi na sita (16) ya SSIDP iii (Small Scale Irrigation Development Project) ambapo kwa Mkoa wa Lindi imetekelezeka miradi mitatu ambayo ni wa skimu ya umwagiliaji Kinyope, Nanganga na Ngongowele Wilayani Newala



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post