Mbunge wa Jimbo la Hanang' Mkoani Manyara, mhandisi Samwel Hhayuma
akizungumza na wananchi wa eneo hilo kwenye sherehe na ibada ya
kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa na wananchi wa eneo hilo kwa kumpa
kura nyingi za ndiyo na kushika nafasi hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Hanang' Mkoani Manyara mhandisi Samwel Hhayuma
(wapili kulia) akiwa na viongozi wa dini na viongozi wa Serikali
kwenye sherehe na ibada ya kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kushika
nafasi hiyo.
Na Mwanashi wetu, Hanang'
MGUNGE wa Jimbo la Hanang' Mkoani Manyara, mhandisi Samwel Hhayuma
amewatoa asante kwa wananchi wake na kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kushika nafasi na kudai kwamba atahakikisha anashirikiana na Serikali kuanzisha viwanda ili kuchakata mazao ya mashamba na mifugo ili
kuongeza uchumi na ajira kwa wananchi wa eneo hilo.
Mhandisi Hhayuma aliyasema hayo katika Mji mdogo wa Katesh, kwenye sherehe hiyo na ibada ya kumshukuru Mungu na kuwapa asante wananchi wa eneo hilo kwa kumchagua kushika nafasi hiyo.
Amewataka wananchi hao kuunga mkono juhudi za serikali za kuleta
maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii kila mmoja katika eneo lake na
kuomba ushirikiano katika juhudi zake za Kutaka kuboresha mifugo,
kilimo na kufanikisha uanzishwaji wa viwanda.
Amesema kwa kushirikiana na serikali ahadi yake ya kutengeneza kiwanda
cha kuchakata nyama ya ngo'mbe katika wilaya hiyo itafanikiwa kwenye
kipindi cha uongozi wake.
Amesema ibada hiyo ni njia mojawapo ya kuchota baraka kutoka kwa
wananchi wake, wazee na viongozi wa dini lakini pia ni fursa ya
kipekee ya kuwaunganisha wananchi wake ili waweze kutafuta kwa pamoja
maendeleo ya wilaya hiyo.
Amesema baada ya kushukuru maana yake unafungua milango mipya ya
baraka waendelee kuomba mafanikio wanaoenda shambani waombe mvua ili
mazao yaliyopo mashambani yasikauke , wafugaji, wafanyakazi wa ofisini
wawe na desturi ya kuomba na mafanikio ya Hanang' ni yetu sote hivyo
washirikiane kwa pamoja kuleta mafanikio.
"Tuendelee kumwombea Rais wetu John Magufuli, viongozi wetu wa
kitaifa, viongozi wa mkoa, wilaya, kata na vijiji ili waweze kufanya
kazi ya kuwatumikia watanzania kwa ufanisi," amesema mhandisi Hhayuma
Paroko wa parokia ya Endasaki Padri Augustino Hhando amesema hakuna
mafanikio yeyote yatakayopatikana bila kumshirikisha Mungu hivyo
waendelee kushirikana na kuiombea safari yake ya kuwatumikia wananchi
iwe ya haki na aongoze kwa hekima.
"Yeye kama kiongozi wa wananchi ametukumbusha sote umuhimu wa
kumshukuru Mungu, hivyo sote tuwe na desturi ya kumshirikisha Mungu
katika kila jambo kwani tunaposali tunajiepusha na hila za muovu
shetani," amesema Padri Hhando.
Sheikh wa Wilaya hiyo Ibrahim Athuman amesema mbunge huyo ameonyesha
hekima yake ya kujali wananchi wake wote bila kujali dini zao itikadi
na makabila hivyo aliwataka wananchi kuendelea kumwombea katika
utekelezaji wake wakiwa katika nyumba zao za ibada.
By Mpekuzi
Post a Comment