Mhubiri Onyebuchi Okocha kutoka Nigeria ambaye alidai kwamba angewafufua wafu siku ya Alhamisi, Januari 28, 2021, amekamatwa na maafisa wa polisi.
Onyebuchi Okocha ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Amafor alikamatwa siku ya Jumatano, Januari 2021, hii ni kwa mujibu wa taarifa za Anambra Broadcasting Servicen nchini humo.
Hata hivyo, nabii huyo ameomba msamaha ingawa serikali ya Anambra imesema itakabiliana naye kisheria kwa sababu anawapotosha wananchi.
Video zake kadhaa zimekuwa zikienezwa mitandaoni zikimuonyesha Nabii huyo akifanya miujiza kadhaa.
Video ya hivi punde, ilimuonyesha mhubiri huyo akiwarushia noti wanaume waliokuwa uchi wakiwa ndani ya mto.
Serikali ya Anambra ilighadhabishwa na video hiyo, maelfu ya wananchi wa Nigeria pia walitoa maoni tofauti wakikashifu vitendo vya mhubiri huyo.
Mhubiri huyo amekuwa akionywa kwa mara kadhaa kuhusiana na vitendo vyake lakini inaonekana hajakuwa akitilia maanani, serikali ya Anambra imeapa kukabiliana naye kisheria.
Via Tuko News
By Mpekuzi
Post a Comment