NAIBU WAZIRI WA FEDHA MHE. MWANAIDI ALI KHAMIS AWAHIMIZA WAHITIMU CHUO CHA MIPANGO KUJIAJIRI |Shamteeblog.

 Na Walace Ng'wandu na Farida Ramadhani, WFM, Mwanza  

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,  amewataka wahitimu wa Vyuo Vikuu nchini wakiwemo wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kutumia vizuri ujuzi walioupata kuleta ufumbuzi wa changamoto za kimaendeleo zinazoikabili jamii pamoja na kutafuta ajira katika sekta isiyo rasmi ili kujiletea maendeleo.

 Hayo ameyasema wakati wa Mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya  Maendeleo Vijijini yaliyo fanyika kwa mara ya 8 katika Kituo cha Kanda ya Ziwa - Mwanza kwa Wahitimu wa Shahada na Stashahada na Astashahada.

 Mhe. Mwanaidi Khamis alisema kuwa hakuna shaka vyuo vinatoa elimu bora ambayo kama ikizingatiwa kikamilifu inatoa fursa ya kujiajiri na kuajiliwa, hivyo kuwa chachu ya maendeleo yatakayoleta tija katika nyanja mbalimbali.

 “Serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuweka mazingira mazuri ya kujiajiri hususani kwa kuboresha mazingira ya kufanya biashara na hivyo kuongeza fursa za vijana wasomi kujiajiri na hatimaye kupunguza tatizo la ajira”, alieleza Bi. Mwanaidi Khamis.

 Alisema kuwa baadhi ya hatua zilizokwisha kuchukuliwa na Serikali ni pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa, kupunguza riba ya mikopo ya mabenki pamoja na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda ili kuongeza ajira na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao yanayozalishwa nchini.

 Naibu Waziri huyo amewaasa vijana wasomi nchini kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi na kuzitumia fursa  mbalimbali zilizopo hususani katika sekta binafsi kujipatia kipato na kuwa na mchango kwa taifa.

 Aidha amekitaka Chuo cha Maendeleo Vijijini kuyafanyia kazi maelekezo ya Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Dkt. Phillip Isdor Mpango aliyoyatoa Jijini Dodoma tarehe 22 Desemba, 2020 alipokutana na Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma ambapo alizielekeza Taasisi za Elimu ya Juu kutumia vyema fursa zilizopo katika kuongeza mapato ya taasisi husika hususani kwa kuimarisha vitengo vya Ushauri na Utafiti ili viweze kuchangia angalau asilimia 10 ili kupunguza utegemezi katika Serikali Kuu.

  Alisema kuwa Chuo Cha Mipango kinatakiwa kuwa mfano kwa Taasisi nyingine za Elimu ya Juu ikizingatiwa kuwa kipo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.  

 Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), Prof. Martha Qorro, alisema kuwa jukumu la taasisi za elimu ya juu hususani Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijini ni kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, maarifa na weledi wa hali ya juu ilikutoa huduma zinazo tatua changamoto za maendeleo katika jamii.

 Alisema kuwa Chuo cha Mipango Tumewezesha kuendelea kutoa mchango kwa jamii kwa kuendesha na kutekeleza miradi ya maendeleo yenye kuwakwamua wananchi wengi kiuchumi hususani katika eneo la mifugo, uvuvi na kilimo.

 Pia alimuahidi Naibu Waziri Mhe. Mwanaidi Khamis kuwa Chuo kinaendelea kupata hati safi ya ukaguzi ambayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali kuanzisha mifumo mbalimbali ya udhibiti, utunzaji, na usimamaizi mapato na matumizi ya fedha za umma.

 Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa -Mwanza Prof. Juvenal Nkonoki, alisema kuwa idadi ya watunukiwa wa tuzo mbalimbali katika mahafali ya 34 yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ni 2571 wakiwemo wanaume 1009 na wanawake 1562.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (MB) akimkabidhi Mhitimu Shaaban Abdala cheti cha mhitimu aliyefanya vizuri zaidi kuliko wahitimu wengine katika hafla ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa - Mwanza.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (MB) akitoa hutuba wakati wa hafla ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza ambapo aliwataka wahitimu wa chuo cha Mipango kutumia ujuzi waliopata kutatua changamo za maendeleo katika jamii ili kukuza uchumi wa taifa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (MB) akimkabidhi cheti cha ufaulu mzuri mhitimu, Hellen Luhunde, katika hafla ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa mkoani - Mwanza.

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakifurahi baada ya kutunukiwa tuzo za shahada mbalimbali na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (MB) katika hafla ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya akielezea historia ya Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa - Mwanza wakati wa hafla ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo hicho.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (MB) na Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho, Prof. Martha Qorro (hayupo pichani), wakati wa hafla ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini yanayofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (MB) (katikati) akiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Martha Qorro (kushoto), pamoja na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Hozen Mayaya katika ukumbi wa mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa - Mwanza.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mafunzo Kanda ya Ziwa Prof. Juvenal Nkonoki akihutubia hadhara ya mahafali ya 34 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika kwa mara ya nane katika Kituo hicho eneo la Bwiru Jijini Mwanza.

(Picha na Farida Ramadhani-Wizara ya Fedha na Mipango, Mwanza)

 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post