Simba SC ya Tanzania rasmi sasa imepangwa Kundi A, Kundi moja na timu za Al Ahly SC ya Misri, AS Vita Club ya DR Congo na Al Merreikh SC ya Sudan katika Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika droo iliyopangwa leo Januari 8, 2021 mjini Cairo nchini Misri.
Katika droo hiyo, Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF Confederation Cup) Namungo FC wamepangwa na timu ya 1º de Agosto ya Angola katika Michuano hiyo.
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kundi B limejumuisha timu za TP Mazembe ya DR Congo, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal Club ya Sudan na CR Belouizdad ya Algeria.
Kundi C kuna Timu za Wydad Casablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea, Atletico Petróleos de Luanda ya Angola na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Kundi D limejumuisha timu za Esperance de Tunis ya Tunisia, Zamalek ya Misri, MC Alger ya Algeria na Teungueth FC ya Senegal.
By Mpekuzi
Post a Comment