Mkurugenzi TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa akiopokea Tunzo ya watu waliotoa mchango mkubwa kwenye jamii iliyotolewa na Zanzibar Youth Awards.
*********************************************
Chama Cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, Zanzibar, (TAMWA ZNZ) tunapenda kumpongeza Mkurugenzi wetu Dr. Mzuri Issa kwa kupata tunzo ya kutoa mchango mkubwa katika jamii kwenye maisha yake. Tunzo hizo zimeolewa na waandaaji wa Tunzo za Vijana Zanzibar (ZYA) hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Mkuu wa jopo la majaji Bw Rashid Mohammed Rashid, alisema mara hii pamoja na kuitoa zawadi kwa vijana wameona pia watowe tunzo kwa watu waliosaidia sana maendeleo ya vijana nchini.
Wengine wanne walipewa tunzo hizo ni Daudi Kombo Maalim, Shaib Ibrahim Mohamed, Raza Lee na DJ Saleh katika ghafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana Mh Tabia Mwita huko Michenzani Mall jana usiku.
Dr. Mzuri amepata tunzo hiyo kutokana na kuwawezesha vijana wanawake katika nyanja mbali mbali za kimaendeleo.
By Mpekuzi
Post a Comment