Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katibu wa chama cha Chama cha Soka mkoa wa Njombe (NJOREFA) Vicent Majiri amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya Anglikana iliyopo Njombe mjini alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia Alfa majiri ambaye ni mdogo wa marehemu,anasema marehemu alipelekwa hospitali January 24 akisumbuliwa sukari na pressure.
“Kakaangu alipelekwa kituo cha afya juzi akisumbuliwa BP pamoja na kisukari,mapaka umauti unamkuta madaktrari wamesema sukari na BP ilikuwa inamsumbua”alisema Alfa
Ameongeza kuwa “Marehemu alikuwa mwanamichezo na aliisaidia timu kadhaa kupanda ligi ikiwemo ndanda ya mtwara na Njombe mji ya hapa mjini Njombe kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kusafirisha mwili ambapo tunatarajia kusafirisha kesho kwa ajili ya mazishi mkoani Mtwara”aliongeza Alfa
Hussein Mwaikambo ni mwenyekiti wa kamati ya mpito ya Club ya Njombe mji fc anasema alifika hospitali alipolazwa kumjulia hali na kudai kwamba ameguswa na kuumizwa na kifo cha kiongozi huyo aliyekuwa na maono ya mbali na soka.
“Jana kwa dakika chache nimebahatika kukutana naye baada ya kupata taarifa kuwa anaumwa,kwa kweli hali yake haikuwa ya kukataisha tama lakini kifo Mungu nio anayepanga na wakati wake ulikuwa umeshafika kikubwa ni kumuombea Mungu amrehemu”alisema Mwaikambo
Baadhi ya mashabiki wa wapenzi na wa soka mkoani Njombe akiwemo Ditram Mbunda wamegubikwa na simanzi huku wakimzungumzia Majiri enzi za uhai wake na mchango wake katika soka la vijana na wanawake na kwamba pengo lake halitozibika.
“Tumeondokewa na mtu mwanamichezo mwenye matajio makubwa na mpira wa Njombe kwasababu tulikuwa tunaongea naye kwa kweli alikuwa na malengo makubwa sana”alisema Mbunda
By Mpekuzi
Post a Comment