Waziri wa Nishati Dkr Medard Kaleman, akizungumza kwenye kituo cha kupokea umeme,kusambaza na kupoza kilichopo eneo la Bulyanhuru wilayani Kahama, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kasimu
“Rais John Magufuli ameshatoa fedha ili wananchi wasambaziwe huduma ya umeme yakiwamo na maeneo ya migodi midogo, hivyo naagiza Januari 3, 2021, watu wa Survey wawe wameshafika kwenye eneo hili la mgodi wa Nyangalata na kuanza mchakato wa kuleta huduma ya umeme hapa, pamoja na kwenye mgodi wa Tambarare,” amesema Dk. Kalemani.
“Lengo la Rais Magufuli ni kuwakuza wachimbaji wadogo, ili wachimbe madini kwa ufanisi, na kuongeza kasi ya uzalishaji wa madini na kupata mapato mengi, na hatimaye kukua kiuchumi na taifa kwa ujumla, na mkitumia umeme mtaokoa gharama ya asilimia 80 ya uzalishaji madini ambayo mnaingia kwa sasa na kutumia Shilingi Milioni 800 kwa mwezi,”ameongeza.
Pia amesema Serikali hadi kufikia Februari 5, mwaka 2021, wanatarajia kuanza kusambaza pia huduma ya Nishati ya umeme kwenye vitongoji na vijiji vyote nchi nzima, ambapo katika wilaya ya Kahama vimesalia vijiji 147, na Halmashauri ya Msalala kuna vijiji 60.
Ziara ikiendelea kwenye kituo cha kupokea umeme, kusambaza, na kupoza katika eneo la Bulyanhulu.
By Mpekuzi
Post a Comment