Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Rogers Machaku akizungumza wakati wa mkutano huo |
AFISA Uhusiano Msaidizi wa Tanga Uwasa Anna Makange akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa kwenye mkutano huo |
ZAIDI ya Bilioni 8 zinatarajiwa kutumika katika mradi mkubwa kuongeza uzalishaji wa maji Jijini Tanga kutoka lita za ujazo 30 kwa siku hadi kufikia lita 45 kwa siku utakaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga Uwasa) kupitia wataalamu wake.
Hayo yalibainishwa leo na Msimamizi wa Mradi kutoka Tanga Uwasa Adela Mboya wakati wataalamu wa mamlaka hiyo walipokuwa wakitoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Kiomoni Jijini Tanga kutambulisha mradi huo ambao utakuwa ni wa kuboresha hali upatikanaji wa maji safi katika Jiji hilo.
Alisema kwamba mradi huo utakuwa ni wa miezi 12 na utakuwa na manufaa makubwa mawili katika mji wa Tanga la kwanza wananchi upatikanaji wa maji ya uhakika ambayo hayakatikikatiki na maji yatapatikana maeneo yote masaa 24.
Alisema pia wakati wa utekelezaji mradi vijana watanufaika kwa sababu watakwenda kuongeza machujio mawili kwenye mtambo wa kusafishia maji uliopo mowe Pande.
Aidha alisema hivyo kazi ya ujenzi kubwa itakayofanyika na kuna tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni 1 na watakwenda kujenga jengine lenye ujazo wa lita milioni 1 eneo la Pande .
Alisema kazi nyengine watalaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 kwa urefu wa kilomita 12.5 kutoka mowe mpaka Kange Jeshini na kwenye tenki hilo bomba litakuwa na kazi ya kusafirisha maji wanayoyazalisha na watakiwa na mabomba mawili makubwa ya kupelekea maji Tanga.
“ Hivyo vijana watanufaika kwenye kazi za ujenzi kuchimba mitaro kwani kwenye mikataba ambayo wataingia na wakandarasi kwamba kazi yoyote ambayo haihitaji wataalamu maalumu inatakiwa itoke sehemu ya mradi Kata ya Kiomoni”Alisema
Aliongeza kwamba hivyo vijana wajitokeza kwa wingi kupata hizo ajira za muda huku akiwaomba wananchi kuwa tayari kupokea mradi na kutoa ushirikiano wakati ukitelekezwa kwenye maeneo yao .
“Kutokana na hilo ndio maana tumepanga kufanya mradi wa kuongeza miuondombinu ya kuzalisha maji kutoka mita za ujazo elfu 30 mpaka elfu 45 kwa siku na mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu”Alisema
Awali akizungumza katika mkutano huo,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Rogers Machaku alisema wanaboresha kwa kiasi kikubwa mtambo wa Mowe hatua ambayo itasaidia kuongezeka kwa maji yanayozalishwa .
Alisema pamoja na kuboresha lakini wanachangamoto ya bomba linalotoka Mowe kwenda mjini eneo la Kange hilo bomba limezidiwa na uwezo hivyo wanataka kuweka mabomba yawe mawili ambao yote yatakuwa yakipeleka maji mjini.
Naye kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kiomoni (CCM) Mohamed Mfundo aliishukuru Tanga Uwasa kwa kufika kwenye Kata hiyo huku akieleza Kata hiyo ndio eneo ambalo mamlaka hiyo imewekeza kwa kiasi kikubwa lakini ni jambo la aibu kwamba baadhi ya maeneo yao hakuna huduma ya maji lakini kwenye maeneo mengine Jijini humo kuna maji.
Alisema analizungumza hilo makusudi kwqa sababu mmefika eneo hilo mtaona namna ya kulifanyia kazi ili kuweza kuondosha changamoto kwenye maeneo ya Masaini,Mijihoroni,Misufini hayo maeneo kuna watu wanaishi na huduma ya maji ni ya kwanza.
“Bila maji hakuna chakula,hakuna mimea,uhai wa chochote hivyo naombeni hizi changamoto mzichukue muende kuzifanyia kazi hilo ni ombi langu kama kiongozi wa Kata mlichukue muone ni namna nani mnaweza kuwapa huduma maeneo yenye changamoto hizo“Alisema Diwani huyo.
By Mpekuzi
Post a Comment