DK KALEMANI : BWAWA LA NYERERE KUANZA KUJAZWA MAJI YA UZALISHAJI WA UMEME WA MEGAWATI 2,115 NOVEMBA 15, MWAKA HUU |Shamteeblog.


Na John Nditi, Rufiji

WAZIRI wa Nishati ,Dk Medard Kalemani amesema Bwawa la kufua umeme wa megawati 2,115 wa Julius Nyerere (JNHPP) litaanza kujazwa maji kuanzia Novemba 15, mwaka huu na hadi kufikia Aprili 15, 2022 litakuwa limejazwa ili mwezi mmoja baadaye umeme uanze kufuliwa kutoka kwenye bwawa hilo.

Dk Kalemani, alisema hayo na kutoa agizo hilo Februari 21, 2021 alipombelea mradi huo kwa mara ya 14 tangu ulipoanza katika wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ili kukagua shughuli mbalimbali zinazoendelea ambapo mbali na kulidhishwa na maendeleo ya ujenzi, alitaka wafanyakazi waongeze haraka.

Hivyo , Waziri huyo amwagiza mkandarasi wa mradi huo kutoka nchini Misri pamoja na Msimamizi wa mradi huo Tanesco kuhakikisha shughuli zote za maandalizi ziwe zimekamilika mapema sana kabla ya Oktoba mwaka huu ili ujazaji wa maji kwenye bwawa uanza Novemba 15, mwaka huu.

Dk Kalemani, alisema hayo na kutoa agizo hilo Februari 21, 2021 alipombelea mradi huo kwa mara ya 14 tangu ulipoanza katika wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ili kukagua shughuli mbalimbali zinazoendelea ambapo mbali na kulidhishwa na maendeleo ya ujenzi, alitaka wafanyakazi waongeze haraka.

“Hizi ni habari njema kama tunafikia kuona tunaanza kujaza maji kwa ajili ya kuanza kufua umeme ni faraja kwetu , lakini kwa leo ninaagiza kwa mkandarasi na hili ni agizo mahususi mkandarasi asimamiwe akamilishe kazi hii haraka ndani ya mpango kazi wake “ aliagiza Dk Kalemani.

Pamoja na hayo Waziri Kalemani ,alisema kuwa bwawa hilo litakuwa na kimo cha mita 131, urefu wa mita 1,125 na ujazo wa mita bilioni 32.5 za maji.

Katika suala hilo Dk Kalemani alitoa maagizo matatu kwa mkandarasi wa Arab Contractors na Elsewedy Electric kutoka Misri ayajenga mradi huo kuongeza idadi ya wafanyakazi , kuleta vifaa vya kutosha vya kufanya kazi ndani ya muda kabla ya ujazaji wa maji kuanza kwa bwawa hilo na kufanya kazi usiku na mchana.

“ Hapa panapo jengwa bwawa hili alate wafanyakazi wakutosha kwani sijaridhika na idadi ya wafanyakazi waliopo ninataka kuona kazi hizi zinafanyika usiku na mchana “ aliagiza Dk Kalemani.

Dk Kalemani , alimtaka msimamizi wa mradi huo kuhakikisha anamsimamia mkandarasi ili kuona bwawa hilo linajazwa maji ndani ya mkataba na si anayotaka yeye ya kulijaza hadi Desemba mwakani , jambo hilo halitakupalika hivyo lijawe hadi Aprili 2022 na si vinginevyo.

Hata hivyo alihoji kuhusu maelekezo yake aliyoyatoa juu ya mapitio ya mpango kazi wa mkandarasi ili aweze kufidia muda unaopotea wa siku 10 hadi 15 , lakini chakushangazwa bado mpango kazi huo hajafikishiwa.

“ Mmemweleza nyie lakini mmeniambia hawezi kuuleta na kama hawezi kuuleta anafanyanini hapa na wewe Mhandisi Mkazi wa Mradihuu nimekuambia una mmamlaka kwenye mkataba “ alisema Dk Kalemani.

Waziri Kalemani, alisema Mhandisi mkazi wa mradi huo, anaouwezo wa mkumkataa kiongozi wa wakandarasi ( Mohammed Hassan ) kwa kuwa yeye (waziri) hajaidhishwa na ufanyakazi na utendaji wa kiongozi wa wakandarasi,kwani hakuna na shida na wakandarasiwengine bali ni kwa kiongozi wao .

“ Ndiyo maana nimeelekeza mpitieni makataba mmkatae kwa dalili hii hatuwezi kufika na taka kuona nikataporudi hapa Aprili mwaka huu nisimkute , nikute msimamizi mwingine bosi wao mwingine anayeweza kuwasimamia kwenda mbele , hawezi kwenda tofauti na makubaliano ya mkataba na sitaki kuona mkandarasi anapingana na maelekezo ya mwajiri wake “ aliagiza Dk Kalemani.

Hata hivyo , alisema tayari Serikali kumlipa mkandarasi trilioni 1.902 hadi kufika Februari mwaka huu ambayo ni asilimia 100 ya malipo ya mpango kazi wake ambapo mradi huo umapangwa kukamilishwa ifikapo Juni 14, 2022.

Katika hatua nyingine Dk Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kuanza ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme 400kv kutoka Bwawa la Nyerere Rufiji hadi Chalinze ili mradi utakapo kamilika umeme uweze kusafirishwa na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Kwa upande wake Kaimu Mhandisi mkazi wa mradi huo, Emmanuel Mwandambo alimhakikishia Waziri Dk Kalemani kuwa maagizo yote atayasimamia kikamilifu ili kuwezesha kufikia malengo ya kukamilishwa kwa mradi huo ifikapo kipindi hicho.

Dk Kalemani , alisema wataalamu muhuhimu ambao bado hawajafika ni wapatao 27 , ambapo aliwataka wafike ndani ya mwezi huu ( Sept ) kwenye ujenzi wa bwawa la Nyarere la kufua umeme wa megawati 2,115 ili kuongeza kasi ya ujenzi ili ukamilishwe kwa wakati ifikapo Juni 14, 2020. “Kwa ujumla ujenzi wa mradi huu wa kitaifa unaendelea vizuri isipokuwa kuna baadhi ya maeneo yatakiwa kuwekewa mkazo hivyo nimemuagiza mkandarasi kuhakikisha wafanyakazi kutoka Misri wanakuja haraka kwenye mdari huu hapa”alisema Dk Kalemani.

Waziri wa Nishati ,Dk Medard Kalemani ( mbele) akielekea kuona  eneo panapojengwa Bwawa la kufua umeme wa megawati  2,115  wa Julius Nyerere (JNHPP) katika  wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani mnamo  Februari  21, 2021 alipofanya  kwenye mradi huo.

Eneo  panapojengwa Bwawa la kufua umeme wa megawati  2,115  wa Julius Nyerere (JNHPP) katika  wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.
 Eneo la ujenzi wa power house.
Waziri Nishati ,Dk Medard Kalemani  ( kulia) akikagua panapojengwa   daraja kubwa katika mto Rufiji kwa ajili ya kupitishwa kwa vifaa vya ujenzi wa bwawa hilo.
Waziri Dk Kalemani  ( wa kwanza kushoto mwenye miwani) kukagua baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi huo.
Baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi Julius Nyerere (JNHPP)  ( Picha na John Nditi).
Waziri Dk Kalemani( wa kwanza kushoto)   akipata maeleo kutoka kwa Kaimu Mhandisi mkazi wa mradi huo , Emmanuel Mwandambo.
Baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi Julius Nyerere (JNHPP)  ( Picha na John Nditi).

 

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post