FEDHA ZA TASAF ZAMPA MTAJI WA BIASHARA YA MCHELE MLENGWA |Shamteeblog.

 

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

MLENGWA wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wilayani Igunga Mkoani Tabora Vivian Makala amefanikiwa kujenga nyumba ya kuishi, kusomesha watoto baada ya kupata fedha za ruzuku ya TASAF na kuanzisha mradi wa kuuza mchele.

Mlengwa huyo alitoa ushuhuda huo jana wakati ziara ya mfunzo ya viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na waandishi wa habari walipokuwa  kujifunza mafanikio ya walengwa yaliyotokana na fedha hizo.

Makala alisema baada ya kupata fedha za TASAF  alianza kwa kukunua gunia mmoja ya mpunga na kulikoboa ambapo alipata kilo 60 alizoziuza kwa shilingi 1,800 kwa kilo na kupata 108,000/= ambazo zilimwezesha kupata mtaji wa kuboresha biashara ya uuzaji mpunga.

Alisema hatua hiyo ilimfanya kutumia fedha hizo kumkopesha mkulima wa mpunga aliyezitumia kulimisha katika mbuga yake na kuzirejesha kwa kumpa gunia 23 baada ya kuvuna  na ndipo hapo mtaji wake uliongezeka.

Makala alisema kutokana fedha anazopata kutokana na mauzo ya mchele amefanikiwa kununua eneo na kujenga nyumba ambayo ndio anaishi.

Alisema faiada nyingine aliyoipata ni pamoja na kusomesha watoto wake kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile sare, viatu na maftari na kuwa na uhakika wa watoto wake kula milo mitatu kwa siku.

Makala aliongeza kuwa fedha anazopata kutokana na mauzo ya mchele zimekuwa pia zikimsaidia katika matibabu yake ya ugonjwa wa miguu ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya asiwe na uwezo wa kusimama kwa muda mrefu.

Alisema tatizo hilo limemfanya kushindwa kujishughulisha na shughuli za shambani na hivyo kupata mtaji huo kumemsaidia kuweza kupata mahitaji yake ya kila siku.

Mlengwa huyo alisema ni vema kwa walengwa wanapata ruzuku kupitia mpango huo kutumia fedha wanazopewa katika shughuli za uzalishaji mali kwa  lengo la kujiua kiuchumi na  kuachana na umasikini na wasirudi nyuma .

Mlengwa huyo alisema hata akitolewa katika Mpango huo hawezi kushindwa kujimudu yeye na familia yake katika m mahitaji mbalimbali.

By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post