RC NDIKILO ANG'AKA FREM 250 KUFUNGWA KISA USHURU USIO RAFIKI LOLIONDO MNARANI |Shamteeblog.

 





MKUU wa mkoa wa Pwani  mhandisi Evarist Ndikilo ametoa siku tatu kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha kukaa meza moja na wafanyabiashara wa soko la Loliondo Mnarani kuona namna watakavyopunguza gharama za ushuru wa frem kutoka sh.8,000 hadi sh.3,000 kwa scale meter moja kwa mwezi.
Hatua hiyo inakwenda kuokoa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakipotea kama mapato ya ndani, kutokana na halmashauri kutoza tozo ya sh .8,000 hali iliyosababisha frem 250 kufungwa kati ya frem 338 zilizokuwepo.

Ndikilo ametoa maagizo hayo baada ya mwenyekiti wa soko la Mnarani ,Mohammed Mnembwe kulalamikia kulipa tozo isiyokidhi pato la mfanyabiashara mnyonge.

Ndikilo alisema hadi kufikia jumatano 24 Februari mwaka huu ,apewe taarifa kuwa wamefikia wapi ili kuhakikisha halmashauri inapata mapato na wafanyabiashara hawakandamizwi ili waliofunga frem zao waweze kufungua.

"Hii itakuwa haiingii akilini, yaani frem 88 tu ndio zinaingiza mapato kisa eti mlipwe tozo kubwa kwa vibanda vichache ,na vile 250 vinafungwa kisa gharama kubwa ,!!kwanini msikae chini kupanga tozo rafiki ili halmashauri inufaike na wafanyabiashara waendelee na biashara zao. "

"Kufikia jumatano nahitaji majibu na nione tatizo hili limekwisha ,na nitakuja hapa kinyemela maana huwa nakuja kuja ,nitajua kama changamoto hii imekwisha ,haiwezekani kila kiongozi wa juu akija kero ni vibanda,frem mara tozo ,ifikie mwisho,!" Mkurugenzi mama Jennifer Omolo naomba usimamie hili "alisisitiza Ndikilo.

Akizungumzia wananchi 23 wanaodai fidia ya eneo hilo amesema kwamba, anatambua watu nane waliopo katika makaratasi toka mwaka 1984 lakini watu 23 walioibuka sasa kutaka kupora eneo hilo la serikali hawatambuliki.

Ndikilo alieleza, watu hao 23 sio wakazi halali wa hapo ni wapya na kama wataona wanaonewa waende mahakamani.

" Mkurugenzi hawa nane wanaosomeka katika makaratasi ndio wapewe maeneo ,tena bure kiwanja kimoja kilichopimwa eneo la Zegereni lakini hawa wengine hawatambuliki. "alikazia Ndikilo.

Nae mfanyabiashara Isack Mfangavo na Ally Pazi ,wakitoa malalamiko kwa mkuu wa mkoa huyo ,walisema mitaji yao ni midogo hivyo gharama za kodi na ushuru viangaliwe na ziendane na wafanyabiashara wanyonge.

Akipokea maagizo hayo ,mkurugenzi wa halmashauri ya Kibaha Mji ,Jennifer Omolo alianisha kwamba,yeye anahoja ya kukaguliwa kuhusiana na mapato ya halmashauri, " Ninapimwa kulingana na ukusanyaji wa mapato ,na eneo lenye maduka mengi ni hapa tunapaswa kukusanya milioni 160 lakini hadi sasa tuna milioni 50 pekee.

Alifafanua , kama wafanyabiashara hao wamekuja na hoja hiyo mpya ,haina shida ameipokea na watakaa mezani.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post