TAASISI YA BETTER HOPE FOUNDATION YAZINDUA KAMPENI YA NIVALISHE, YAOMBA JAMII KUSAIDIA WATOTO WENYE MAHITAJI |Shamteeblog.

Mkurugenzi wa better hope Fondation Maziku Kuwandu katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutambulisha kampeni ya NIVALISHE kwaajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu hasa wa vijijini kushoto ni afisa mawasiliano wa taasisi ya better hope Fondation, Agness Maliki na kulia ni Meneja mipango wa taasisi ya better hope Fondation, Peter Elias Masoi.
 Afisa mawasiliano wa taasisi ya better hope Fondation, Agness Maliki

TAASISI isiyo ya kiserikali ya better hope Fondation katika kuisaidia jamii imezindua kampeni ya NIVALISHE kwaajili ya kusaidia watoto wenye uhitaji hasa waishio katika mazingira magumu na yatima.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa better hope Fondation Maziku Kuwandu amesema kuwa katika kutekele moja ya majukumu ya taasisi ya better hope Fondation ni kuwasaidia na kuwatemeelea watoto yatima waliopo hapa nchini.

"Mategemeo ya Kampeni hii ni kuwafikia watoto wa vijijini hasa wa mkoa wa Pwani na kuwapatia mahitaji ya msingi hasa mahitaji ya shule na kubadilisha mitazamo hasi, kuwaongezea kujiamini, kuvalisha ujasiri na kutoa elimu ya malezi kwa wazazi na walezi ikiwa ni njia moja wapo ya kusaidia jamii hasa kipindi hiki cha Kwalesima tujitoe kwaajili ya mtoto mwenye mahitaji." Amesema Maziku.

Amesema kuwa taasisi hiyo ipo kwaajili ya kuhamasisha jamii ili kuweza kujitoa kwaajili ya watoto waishio katika mazingira magumu hasa vijijini.

"Pia tuna programu yetu ya TUONGEE MALEZI YA MTOTO kwaajili ya kuwasaidia watoto waweze kutimiza ndoto zao." Ameongeza Maziku.

Kupitia NIVALISHE Kampaign pia wametambulisha JEROFUND kama sehemu ya kuiwezesha jamii kuweza kuchangia mia tano ili kufanikisha malengo ya taasisi ya better hope Fondation.

"Sisi kama jamii tunawajibu wa kusaidiana hivyo nihamasishe jamii kwa ujumla kuweza kuchangia chochote mtu alichonacho ili tuweze kwenda kuwapelekea watoto wenye mahitaji sote kwa pamoja na taasisi ya better hope Fondation".

"Shukrani zetu za dhati kwa wadau wetu walioweza kuungana na sisi ambayo ni Techo tz, Farry Bizz, Nilee foundation, lambokile Company Ltd, Update your brain , The Event ~Corps , JJm boutique, Jaxstore , S.s virtous Finance co.Ltd." Amesema Maziku


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post