WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BIDHAA ZA VIWANDA VYA NDANI |Shamteeblog.


  Afisa uhusiano na Meneja Masoko wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd,)  Fredrick Njoka akitoa maelekezo ya bidhaa ambazo wanatengeneza kwa wananchi  waliotembelea katika banda lao akiwemo mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Anna Mghwira  akiangalia viatu wakati akitembelea banda la International Leather Industries Co. Ltd)  lililopo Katika maonesho ya nne ya programu ya uwezeshaji kiuchumi wananchi yanayofanyika Katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.


 Na Woinde Shizza Michuzi Tv - ARUSHA


WATANZANIA wametakiwa kupenda na kutumia bidhaa  zinazozalishwa  nchini  zikiwemo bidhaa za ngozi zinazozalishwa na kiwanda cha Kilimanjaro kinachozalisha bidhaa zenye ubora  wa kimataifa .

Hayo yamebainishwa na Fredrick Njoka  ambaye ni Afisa uhusiano na Meneja Masoko wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd) wakati wa maonesho ya nne ya mifuko ya baraza la uwezeshwaji kiuchumi na kueleza kuwa kiwanda hicho  kinamilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza.

Njoka amesema, Watanzania wanatakiwa kujua kuwa kauli mbiu ya  Tanzania ya viwanda ni pamoja na kupenda na  kuunga mkono vitu na bidhaa zinazotengenezwa na viwanda vya Tanzania na kuhamasishana watanzania wenyewe kwa wenyewe kupenda vitu vya ndani. 

Amesema kuwa kiwanda hicho kimesaidia upatikana kwa soko la uhakika la ngozi ghafi kutoka kwa wafugaji, Kuongeza thamani ya ngozi inayozalishwa hapa nchini kutokana na mpango wa mafunzo maalumu kwa wafugaji na ajira za moja kwa moja 3000 na zaidi ya ajira 7000 zisizo za moja kwa moja katika mnyororo wa thamani na huduma.

Amesema kiwanda hichi kinasaidia  kuongeza mapato kwa Taifa kupitia kodi mbalimbali.

 "Pia kiwanda hiki kina manufaa makubwa kwa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wakazi, majengo na miundombinu na kinaokoa fedha za kigeni kwa kupunguza uingizaji wa bidhaa za ngozi nchini na kuongeza mapato ya fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa za ngozi nje ya nchi.'' Amesema.  

 




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post