DIWANI KATA YA SEKEI JIJINI ARUSHA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE |Shamteeblog.

 Na Woinde Shizza,ARUSHA


Diwani wa kata ya sekei mkoani Arusha Gerald John Sebastian ameanza kutekeleza ahadi aliyoitoa katika majukwaa ya kampeni ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa mkopo wa shilingi million moja wanawake 20 wa mtaa wa  Sanawari ili kuweza kukuza mitaji yao.

Akikabidhi mikopo hiyo Sebastian alisema kuwa Kata yake ina mitaa 6 na wakati wa kampeni aliahidi kutoa fedha za kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kukuza  mitaji yao ambapo kwasasa ameanza na mtaa wa Sanawari na ataendelea na mitaa mingine.

“Nimeanza na hawa ishirini kwa sasa lakini wanatakiwa kurejesha ili na wengine kwenye mtaa wao waweze kupata na mitaa mingine nitaenda kufanya hivi hivi na ni imani yangu mtaenda kufanya tuliyoyakusudia” Alisema Sebastian.

Alieleza kuwa fedha hizo zitakaporejeshwa hazitarudi kwenye mikono yake bali zitawafikia wanawake wengine wenye mazingira  magumu ya upatikanaji wa mitaji katika kuendeleza biashara zao ili kujikwamua kiuchumi ambapo mikopo hiyo haina riba.

“Ndani ya miaka mitano naamini  nitaweza kuwasaidia wanawake 5000 na fedha hizi sio msaada bali wakazitumie katika kuendeleza miradi yao midogo midogo kwa kuongeza mitaji katika biashara zao lakini pia niwasihi wasivunjike moyo kwani kuna wafanyabiashara wakubwa walioanza na mitaji kama hiyo,”Alieleza.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuhiya ya umoja wa wanawake wa jiji la Arusha(UWT) Marry Kisaka aliwataka wanawake kufanya kazi kwa bidii ba malengo kwani kwa asilimia kubwa wanawake  wanategemewa na familia jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa Diwani huyo amekuwa mfano kwa madiwani wengine wote kwani ametekeleza yale aliyoyaahidi bila kusuviri msaada wa chama wala serikali kuu na jambo hilo linawafanya wananchi kuzidi kukipenda na kukiamini chama.

“Kupitia fedha hizi mwanamke akijipanga vizuri katika kufanya kazi ataondokana na utegemezi na kuinuka kiuchumi kwani fedha hizi sio ndogo, mimi mwenyewe  nilianza na mtaji wa sh.50000 lakini hivi sasa nazungumzia   milioni 20 hadi 30 hivyo msidharau hichi kidogo mlichokipata bali mkasimame imara katika kufanya kazi,”alisema Merry Kisaka.

Naye afisa maendeleo ya jamii wa kata ya Sekei  Mecy Urasa alisisitiza kuwa mikopo hiyo iwe chachu ya kuleta maendeleo katika familia na jamii kwa kuendeleza miradi yao midogo midogo ili kuleta tija kwa jamii kwani kwa kuunda vikundi ni njia pekee ya kuwezeshwa kupata mikopo.
 
 Diwani wa kata ya sekei uliopo ndani ya halnashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha Gerald John Sebastian akikabidhi fedha za mkopo mmoja wa kinamama wa kata ya sekei hii ikiwa ni ukutekeleza ahadi aliyoitoa katika majukwaa ya kampeni ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa mkopo wa shilingi million moja wanawake 20 wa mtaa wa Sanawari ili kuweza kukuza mitaji yao (picha na Woinde Shizza , ARUSHA)
 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post