MAABARA YA TMDA NAMNA INAVYO CHUGUZA VIFAA TIBA NA KONDOMU |Shamteeblog.

WAANDISHI wa vyombo vya habari Mkoa wa Dar es Salaam wamefanya ziara maalum  katika  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA) kwa lengo la  kujifunza na kuongeza uelewa wa  kuona ni namna gani Vifaa Tiba na Dawa zinavyochunguzwa na mashine na kutambulika kuwa zinau bora.

Akitoa utangulizi kabla ya kuanza  kwa ziara hiyo Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza amesema kuwa ziara ya mafunzo hayo yatafanyika  siku tatu ambapo yatawaongezea uelewa  waandishi hao katika masuala ya Dawa na Vifaa Tiba  kujua namna maabara hizo zinavyoweza kuthibitisha ubora.

Simwanza amesema kwa siku ya kwanza ya ziara hiyo ya  waandishi hao wanapata fursa ya kutembelea maabara ya Vifaa Tiba na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo inayochunguza bidhaa za kondom.
 
Kwa upande wake Mchunguzi wa Maabara hiyo,Saxon Mwambene ameelezea aina za  mashine zinazo pima ubora katika bidhaa hizo za Kondomu na Gloves.

Amesema kuna mashine mbalimbali za kupima bidhaa hizo ikiwemo Mashine ya mashimo madogomadogo ya Kondomu  (ELECTRIC LEAK TESTER FOR CONDOMS), Mashine ya kuangalia ubora wa vifungashio (AUTOMATED WET PACKAGE SEAL INTEGRITY TESTER FOR CONDOMS), Mashine ya kupima ubora wa Gloves na Kondom za Kike (VISUAL LEAK TESTER FOR GLOVES / CONDOMS), Mashine ya kupima ukubwa wa Kondom (AUTOMATED WIDTH TESTER), na Mashine ya kupima uimara wa Kondom (AUTOMATED INFLATION SYSTEM).
 
Aidha Mtaalamu huyo ameongeza kuwa kazi wanayoifanya ya kupima ubora wa bidhaa hiyo ni kazi ya kisayansi. Hivyo wanajukumu la kufanyakazi hizo kwa umakini mkubwa na udalifu kwani wanatambua kuwa jamii ya watanzania wana imani kubwa na TMDA katika kupima na kuthibitisha bidhaa zote za vifaa Tiba na Dawa kabla hazijawafikia wananchi.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza (kulia)akizungumza na waandishi wa habari namna mashine za kupima ubora zinavyo fanya kazi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya  habari wakimsikiliza Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza (katikati)
Mtaalam wa Maabara ya TMDA Saxon Mwambene (wapili kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari namna Mashine zilizopo kwenye Maabara hiyo zinavyofanyakazi ya kupima bidhaa hizo (kwanza kulia) Happyness Seswa.
 Mtaalam maabara ya  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Happyness Seswa kulia akiendelea na kazi ya kuwaelimisha waandishi wa habari namna maabala hiyo inavyofanya kazi .(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post