MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umepungua kutoka asilimia 3.5 kwa Mwaka ulioishia mwezi Januari ,2021 hadi kufikia asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari,2021.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dodoma Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ruth Minja kuwa inamanisha kuwa Kasim ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa Mwaka iliojishika mwezi Februari 2021 umepungua ikiliganushwa na kasi iliyokuwepo kwa Mwaka iliojishika mwezi Januari 2021.
Aidha alisema Kupungua kwa mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umechangiwa hasa nakupungua kwa bei za Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kikichoishia Februari 2021 zikilinganishwa na bei za mwezi Februari 2020.
Alisema Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei kwa mwezi Februari 2021 zikilinganishwa na bei za Mwezi Februari 2020 nipamoja na Thamani,kwa asilimia 5.3, Mafuta ya taa kwa asilimia 15.7 ,Vifaa vya nyumbani kama vile pasi ya umeme kwa asilimia 4.7, vyomboa vya ndani kwa asilimia 3.3 Dezeli kwa asilimia 22.8,Petroli kwa asilimia 13.4.
Hata hivyo alisema mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa mwezi Februari 2021 umeongezeka kutoka asilimia 2.8 mwezi Januari 2020 hadi asilimia 3.6.
Kuhusu hali ya mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa Mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 Minja amebainisha kuwa Nchini Kenya mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umeongezeka kutoka asilimia 5.69 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2021 hadi kufikia asilimia 5.78 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 .
Kuwa nchini uganda mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2021 umeongezeka kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2021 hadi kufikia asilimia 3.8.
By Mpekuzi
Post a Comment